RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FAIDA NA TIBA YA JUISI YENYE MCHANGANYIKO MAALUMU WA MATUNDA





JUISI ni kinywaji bora na maarufu duniani. Hata hivyo, si kila juisi ina faida katika mwili wa binadamu. Kwa hiyo, ni muhimu kutambua ni juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote kabla ya kuinywa.

Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa Juisi, wakati ukweli halisi si Juisi si chochote, bali ni vinywaji vyenye ladha tu ya matunda mbalimbali.

Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama vile Juisi ya Machungwa, Nanasi, Zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za viwandani kwa lengo la kuvihifadhia (Preservatives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki hata kidogo, havina tofauti na sumu nyingine yoyote kama ilivyowahi kuelezwa na wataalamu hapa FikraPevu.

Licha ya Juisi halisi kutumika kama kinywaji, lakini Juisi halisi hiyo hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali mbalimbali mwilini. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalumu wa matunda na kutayarisha Juisi maalumu na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini.

Karoti, Kitunguu swaumu na Apple (TUFAHA)

Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo/apple au tufaha, husafisha sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.

Tufaha, Tango na Figili

Juisi ya mchanganyiko wa tunda la Tufaha, Tango na Mboga ya Majani aina ya Figili (Celery), hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro (lehemu) mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.

Nyanya, Karoti na Tufaha
Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na tufaha huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.

Chungwa, Tangawizi na Tango

Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.

Nanasi, Tufaha na Tikitimaji

Juisi ya mchangayiko wa nanasi, tufaha (epo) na tikitimaji, huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba Juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.

Karoti, Tufah, Peasi na Embe

Juisi ya mchangayiko wa karoti, tufaha, peasi na embe hushusha joto la mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na matatizo ya kupumua.

Papai, Nanasi na Maziwa

Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).

Ndizi, Nanasi na Maziwa

Juisi yenye mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa ina vitamin nyingi na virutubisho vingi vinavyosaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Kwa ujumla, Juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo, ikitumiwa vizuri kama ipasavyo, hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili, na pia huweza kuwa tiba ya magonjwa ya saratani.

Ili uone faida za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi.

Kwa mujibu wa mtandao wa kijamii wa JamiiForums kwenye Jukwaa la Utabibu, wanachama wake wakiwemo wataalamu wa afya wameeleza kuwa Mungu alipomuumba mwanadamu chakula alichokiandaa kwa ajili yake ni kile kinachotokana na mimea yaani matunda na mboga za majani. Vyakula hivi licha ya kuwa chakula pia ni dawa inayotibu maradhi mbalimbali katika mwili wa binadamu. Vyakula vyenye asili ya mimea vikiliwa vikiwa katika hali ya ubichi (raw, uncooked and unprocessed) vinaipa miili viini lishe (Nutritional elements/Enzymes) ambazo hufanya miili kuwa katika uwiano sawa na hivyo kuwa katika afya njema.