Select Menu

News

IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUMAPILI HII

MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" JUMAPILI HII

MTUME DR. PETER NYAGA

MTUME DR. PETER NYAGA

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » GONDWE AKAMATA MALORI SABA YAKISAFIRISHA MADINI USIKU!


Sanga Rulea 1:39 AM 0

Handeni, Tanga;

Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amekamata malori saba yakisafirisha madini ya chuma aina dolomite yanayotumika kutengeneza saruji.

Gondwe amesema kati ya malori saba walifanikiwa kukamata matano, huku mawili madereva wakiwahi kutoroka. “Malori hayo yalikuwa yanatokea Kata ya Mgambo, yanakochimbwa madini hayo,” amesema.

Kufuatia hatua hiyo, Gondwe ametangaza kupiga marufuku usafirishaji madini usiku.

“Tulipokamata magari hayo, kwanza tuliwauliza kama wamelipa kodi na kama wamelipa watuonyeshe stakabadhi,” amesema.

Alisema madini yanapo safirishwa nje ya wilaya mfanyabiashara anatakiwa kuilipa Serikali Kuu asilimia tatu na halmashauri inatakiwa kulipwa asilimia 0.3 ya mauzo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, William Makufwe amesema wamekuwa wakipoteza mapato kupitia wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.

Makufwe amesema wameanza kukusanya kodi kwa kutumia wataalamu wao na kuachana na mawakala, ambao walikuwa wanawasilisha fedha kidogo.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilaya za Handeni na Kilindi, Charles Kamuhanda alisema kumekuwa na changamoto ya ulipaji kodi kutoka kwa wafanyabiashara. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS