MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

GOSPEL STAR SEARCH MGUU KWA MGUU MPAKA KWA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE WA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Waimbaji waliobahatika kuingia katika kinyang'anyiro cha kkumpata mshindi wa kwanza katika mashindano ya Gospel Star Search (GSS) 2016 siku ya Jumapili 11.09.2016, waliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare  kwaajili ya kuoombewa. Waimbaji hawa waliongozwa na mtangazaji wa Chomoza Clouds TV Jimmy Temu ambaye alishawahi kutangaza katika kipindi cha Rise and Shine cha Praise Power Radio. Lengo lao kuu ilikuwa ni kuombewa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwani chimbuko la GSS lilianzia hapo Mlima wa Moto Mikocheni "B" na aliyekuwa mtangazaji wa Praise Power Radio 99.3FM Mch. Harris Kapiga na kundi lake.

Waimbaji hawa walipata muda wa kuimba na baadae waliweza kuombewa tayari kwa kwenda kushindana kupata mshindi wa kwanza siku hiyo ya Jumapili. Kanisa zima liliweza kunyoosha mikono kuelekea kwa waimbaji hawa waliokuwa madhabahuni.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwaomba wazidi kuimba na kumtukuza Mungu kutoka moyoni na isiishie kwenye GSS tu. Wasonge mbele kwa kazi ya Mungu na wakifanya hivyo watafanikiwa katika maisha yao na kazi zao.

Tunakuribisha wewe ambaye umewahi au hujawahi kufika katika kanisa la Mlima wa Moto siku ya Jumapili saa 3 asubuhi. Unaweza kuona matukio yetu katika blogu yetu www.mountainoffiretanzania.blogspot.com/
  Uncle Jimmy Temu


 GSS- Wakijiandaa kuimba