MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HUYU NDIYE MSHINDI WA 500,000/- ZA GAZETI LA AMANI

HATIMAYE! Mshindi wa pili wa Chemsha Bongo katika gazeti hili la Amani amepatikana na kukabidhiwa zawadi yake ya Sh. 500,000. Unajua ni nani? Anaitwa Godwin Deodath Katiali mkazi wa Njia Panda Machame, Moshi mkoani Kilimanjaro.


Mshindi wa pili wa Chemsha Bongo katika gazeti hili la Amani, Godwin Deodath Katiali mkazi wa Njia Panda Machame, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na Amani, kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa zawadi na wakala wa Global Publishers, Moshi mkoani Kilimanjaro, Neema Mbuya wiki iliyopita alisema kuwa imekuwa bahati kubwa kwake na imeweka historia katika maisha yake.


Wakala wa Magazeti ya Global Publishers, Neema Mbuya akimkabidhi zawadi ya shiling 500,000/- mshindi huyo.

“Ujue hii kwangu ni bahati nasibu kubwa ya kwanza kushinda katika bahati nasibu nyingi nilizowahi kucheza. Nimekuwa mdau wa Magazeti Pendwa ya Global kwa kipindi kirefu na pia kushiriki mara kwa mara pindi chemsha bongo zinapotokea,” alisema Godwin.

Akiongelea zawadi yake hiyo ya Sh. 500,000 Godwin alisema anaamini kila kitu kinakuja kwa wakati wake, alikuwa akihangaika kutafuta hela ya kumalizia fremu pamoja na matatizo madogomadogo nyumbani lakini ghafla amejikuta zawadi hiyo ikimdondokea.

“Siyo siri yote namshukuru Mungu. Ujue mimi nina watoto wawili mmoja wapo amemaliza la saba, sasa hii imekuwa kama kulala maskini na ghafla kuamka tajiri. Nawashuruku sana Global kwa kiasi hiki kwangu si kidogo ni kikubwa sana na kitanisaidia kumalizia fremu ambayo ilibakiza bati na sementi kidogo nimalizie,” aliweka nukta Godwin.

Naye Wakala wa Magazeti ya Global, Neema Mbuya aliwaomba wasomaji wa magazeti hayo kusoma kwa wingi na kushiriki chemsha bongo zilizomo katika magazeti hayo kwani ni za kweli.
“Yeyote anaweza kuwa mshindi na kupata kiasi cha Sh.500,000 katika Chemsha Bongo inayopatikana katika Gazeti la Amani. Ni rahisi kwani kwa kiasi cha shilingi 500 unazonunua gazeti unapata bahati ya kujibu swali linalopatikana katika gazeti hilo ukurasa wa pili kisha unasubiri huenda ni wewe,” alisema Mbuya.

Hii ni mara ya pili kwa Gazeti la Amani kutoa mshindi katika chemsha bongo hii, mshindi wa kwanza alikuwa Bakari Omar Omunga mkazi wa Manzese jijini Dar ambaye naye alijizolea kiasi cha Sh. 500,000.
Chemsha Bongo hii bado inaendelea katika gazeti hili. Kushiriki ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti lako la Amani kila Alhamisi na kujibu swali kiufasaha linalopatikana ukurasa wa pili. Kumbuka mshindi pia anaweza kupata safari ya kwenda kwenye jiji la maraha duniani, Dubai kula bata kwa siku tatu.