MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KUNA NGUVU KUBWA KATIKA KUSAMEHE


Mwisho wa somo ili utagundua nguvu iliyopo nyuma ya kusamehe. Kuna watu wanapitia kwenye matatizo na magonjwa kwasababu ya kutokusamehe. 


Mathayo 6:9-12 “basi ninyi salini hivi…12 msipowasamehe wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Zaburi 103:3 Hapa tunaona kuwa kanuni ya Mungu ni kusamehe kwanza kabla ya kuponya. Na ndio maana waweza kumwona mtu anasema ameokoka lakini bado yupo kwenye ugonjwa kwasababu ya kutokusamehe. 

KWANINI UMSAMEHE ALIYEKUKOSEA:

Kumsamehe mtu aliyekuumiza sio jambo la mzaha, na ndio maana kuna watu wanasema kuwa wamesamehe lakini ndani ya mioyo yao bado hajasamehe. Tunatakiwa kusamehe kwasababu kuna nguvu iliyopo nyuma ya mtu aliyekukwaza au kukuumiza.

Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu hawajui nguvu iliyopo nyuma ya yule mtu aliyewakwaza. Emu tuangalie mfano wa gari; Gari linapomgonga mtu serikali haishtaki gari bali anayeshtakiwa ni dereva. Vivyohivyo ukiumizwa unatakiwa uangalie ile nguvu iliyopo nyuma ya aliyekuumiza. Kimsingi kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya aliyekuumiza na usipoijua hiyo nguvu utajikuta unashindwa kusamehe.

VITU VITATU AMBAVYO NI VIPIMO KAMA UMESAMEHE AU BADO HUJASAMEHE:

1. Ukimsamehe mtu utamwongelea vizuri:

Kama kweli umemsamehe mtu utamwongelea vizuri mbele za watu, kama unasema umemsamehe mtu alafu bado unamwongelea vibaya ujue bado hujasamehe kutoka moyoni mwako. Ukimkuta mtu anaongea mabaya kuhusu mtu aliyemkwaza basi ujue ndani ya moyo wake kuna madabahu ya makwazo na machungu. Na kwasababu hiyo kuna watu wamefukuzwa kazi, wamepigwa kwasababu ya kushindwa kuwanenea watu mazuri.


2. Ukimsamehe mtu utamwombea:

Ishara nyingine kuwa ya kuonyesha kuwa umesamehe ni kumwombea mwingine mazuri; na ndio maana Eliya alipotaka kujenga madhabahu ya Mungu alibomoa kwanza madhabahu ya baali, hata leo huwezi kujenga madhabahu ya Mungu ya amani kama bado moyoni unamadhabahu ya kutokusamehe. Watu wengi wamejikuta wakiomba mabaya kwa watu waliowakosea na kwa namna hiyo wanashindwa kupokea majibu ya matatizo yao.


3. Ukimsamehe mtu utawasiliana kwa uzuri:

Ukimsamehe mtu utawasiliana naye kwa uzuri, nah ii ni kwenye madhabahu ya moyo wako. Hata kama amekujibu vibaya wewe mjibu kwa uzuri. Ni kweli kuwa ukisamehe Yule mtu atakudharau lakini ni muhimu kujua kuwa tunasamehe si kwa ajili ya waliotukosea bali kwa ajili yetu.


Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu ya kukosa nguvu ya uwezesho ya kuweza kusamehe. Kila mtu aliyeokoka anayo nguvu ya uwezesho ya kusamehe, nayo ni Roho Mtakatifu. Kila mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu naye hutuwezesha kusamehe, kuokoka kunakupa nguvu ya uwezesho kusamehe. Bila kusamehe huwezi kupokea kutoka kwa BWANA. 


MAOMBI YA KUSAMEHE:

Baba katika Jina la Yesu Kristo ninaomba nguvu ya msamaha wako; leo nimetambua kuna nguvu inayotenda kazi nyuma ya mtu aliyenikwanza, leo ninawasamehe wote walionikwaza katika Jina la Yesu. Ninatangaza msamaha, ninavunja madhabahu ya makwazo na kutokusamahe ndani yangu katika jina la Yesu Kristo. Baba ninaomba uniponye na matatizo yaliyoingia ndani yangu kwasababu ya kutokusamehe katika Jina la Yesu. Leo ninabadilika katika Jina la Yesu. Mimi ni mzima na nimeponywa katika Jina la Yesu.MUNGU akubariki sana