RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MASANJA AGEUKA MHUDUMU WA MISOSI (VIDEO+PICHA)


MCHEKESHAJI wa kundi la Orijino Komedi,Emmanuel Mgaya wikiendi iliyopita aligeuka kuwa mhudumu wa misosi baada ya kuonekana akiwa amevalia vazi la kuuzia vyakula lenye maandishi ya ’Masanja Wali Nyama’.Msanii huyo alionekana katika hafla fupi ya semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyokuwa imeandaliwa na wahamasishaji maarufu Antony Luvanda na Dk. Chris Mauki ambapo alikuwa akihudumia wageni waalikwa sambamba na mkewe aliyefunga naye ndoa hivi karibuni aitwaye Monica.
Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya‘Masanja Mkandamizaji’ akitokelezea na vazi lake lililoandikwa ‘Masanja Wali Nyama’.

Mke wa Masanja aitwaye Monica akiwa na wahudumu wengine wakionesha vyakula wanavyoviuza.


Mke wa Masanja (kulia aliyeko mbele) akinyoosha kidole.


Masanja akiwa na mkewe Monica na nyuma yao ni baadhi ya vyakula wanavyoviuza.



Wakibeba vyakula hivyo.


Wakiendelea kutoa huduma