RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI MELENIA IRENGO WA KANISA LA EFATHA AFUNDISHA SOMO LA TABIA

 Tabia humtambulisha mtu katikati ya watu, tabia yako itakutambulisha kwa watu kuwa wewe ni wa namna gani. Tabia inaweza kumuinua mtu kutoka chini na kumketisha juu. Mfano Mfalme Daudi alikuwa na tabia nzuri tangu akiwa mdogo na Mungu akamuinua kutoka kuchunga kondoo wa Baba yake na kumfanya kuwa Mfalme, tabia nzuri ndiyo inaweza kusababisha ukainuliwa kutoka chini na kuwekwa juu na wafalme. Wagalatia 6:7 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.” Unatakiwa ujitathmini mwenyewe kwanza unapanda nini kwa Mungu au kwa watu ili usije ukavuna usicho kitegemea kwa kuwa ukipanda mazuri ndiyo utakayo vuna na pia ukipanda mabaya ndiyo utakayo vuna, panda mema kwa Mungu au watu ili uvune mema. Rumi 8:14 “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.” ukitaka kutembea na tabia ya Mungu hakikisha unaongozwa na Roho wake maana ukiongozwa na Roho hutafanya yasiyo MPENDEZA MUNGU maana ROHO wa MUNGU ANAKUPA NEEMA jinsi ya kuenenda hapa chini ya jua.


TABIA Tabia ni nini? Tabia ni matendo, mienendo au sifa mbalimbali za mtu zinazoambatana na matendo yake au Nafsi yake. Tabia ziko za aina mbili:- 1. Tabia nzuri: Hii ni tabia inayotoka kwa Mungu. 2. Tabia mbaya: Hii ni Tabia inayotoka kwa ibilisi. Uwe na TABIA NZURI ili watu watamani kuwa kama wewe kwa sababu tabia nzuri INAVUTA watu karibu na wewe. Mfano mzuri ni BWANA wetu YESU KRISTO alikuwa na tabia ya KUWAVUTA WATU ILI WAMJUE MUNGU. Uwe na tabia ya kuwavuta watu ili wamjue Mungu na usiwe na tabia ya kuwakimbiza watu, iwe ni kwa maneno au kwa chochote kile mahali popote utakapokuwepo. Wagalatia 5:16-24 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.......”