RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI WA PENTECOSTE MBARONI KWA TUHUMA ZA RUSHWA



Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Kagera, inamshikilia mchungaji wa kanisa moja la Kipentekoste Bukoba, kwa tuhuma za kutoa rushwa ya shilingi laki moja kwa aksari polisi aliyekuwa akichunguza tuhuma zinazomkabili.

HossanaKwanza.com imefanya mahojiano na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Joseph Mwaiswelo, ambaye pamoja na kuthibitisha kuwa wanamshikilia mchungaji huyo, ametumia nafasi hiyo kuzitaadharisha taasisi zinazogawa bidhaa za misaada kwa waanga wa tetemeko la ardhi Kagera, kujizuia na kuomba rushwa katika shughuli hiyo.



Mvutano juu ya viwanja uliibuka katika eneo la Kyabitembe kata Nshambya katika manispaa ya Bukoba, uongozi ulipotangaza kuendeleza eneo hilo, ingawa ulikumbana na changamoto za udhibiti ununuzi na uuuzaji holela wa viwanja, kati ya mwaka 2010 na 13.

Amesema kuwa upo uwezekano wa ama aliyeathirika au mtathimini kumshawishi mwenzake, hasa kwakuandika athari zilizokithiri au kuingiza jina la asiyeathirika, sambamba na wasambazaji wa misaada kuwanyima waathirika misaada kwasababu tu hawakutoa chochote, kuwa TAKUKURU inaendela na ufuatiliaji wake ili wakibaini tuhuma zozote wachukue hatua mara moja.