RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MARRIAGE REVIVAL DINNER PARTY 2018

MARRIAGE REVIVAL DINNER PARTY 2018

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

MTANGAZAJI CHANEL TEN AFARIKI DUNIA


Cassius Mdami enzi za uhai wake.

MOROGORO: Aliyekuwa mtangazaji wa Channel Ten, kipindi cha Utalii Tanzania, Cassius Mdami amefariki dunia leo katika Hospitali ya Mazimbu Morogoro.

Marehemu alianza kusumbuliwa na maradhi tangu mwanzoni mwa mwaka huu na kupatiwa matibabu jijini Dar es Saalam kabla ya kuhamishiwa mkoani Morogoro, ambako alifikwa na mauti leo mchana akiwa amelazwa hospitali ya Mazimbu iliyopo mkoani Morogoro.

Marehemu enzi za uhai wake alikuwa akitangaza kipindi cha Utalii kinachorushwa na kituo cha luninga cha Chanel Ten, ambacho kwa kiasi kikubwa kimechangia kukuza sekta ya utalii nchini.

Taarifa kamili kuhusu mazishi yake zitatolewa baadaye.

Bwana alitoa na bwana ametwaa, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.