RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NAMNA YA KUJIKWAMUA NA HALI NGUMU YA MAISHA KWA MTU YOYOTE.



Habari za leo ndugu wasomaji

leo nitaelezea jambo muhim sana katika maisha yetu na jinsi gani tunavyojiingiza katika umasikini kwa aibu zetu
ndugu wasomaji kuna vijana wengi wapo mitaani hali ya kuwa hawana shughuli za kufanya wakiishia kulalamika
kua hakuna ajira,maisha magum, na wengine kujikuta wakitumbikia katika majanga ya kutumia madawa ya kulevya,
uporaji na ukahaba sababu tu ya aibu
mimi nina amini kua kila mtu anauwezo wa kufanya jambo fulani au kitu fulani kikampelekea kwenye utajiri au
malengo anayoyataraji ila ibu inamsabaisha mtu uyo asiweze kuendelea na kungangana na kuzidi kudidimia
katika umasikini ndugu zangu sasa ni wakati wa kupambana na maisha na kutekeleza malengo yako yote
uliyo jiwekea bila kujali au kumuangalia fulani atasemaje au atanicheka.

katika pitapita yangu siku moja nilikutana na kijana fulani alikua akilala mika kua maisha magum hakuna ajira na mambo
mengi ya kulalamikia maisha nikamuuliza je amesha wahi kujishughulisha na shughuli yoyote itakayoweza kumuingizia
angalau shilingi mbili tatu akanijibu hapana basi nikampa ushauri kua kwa elim aliyo kuwa nayo kuna kampuni za ulinzi
tena za kisasa wanahitaji wafanyakazi alichonijibu ndugu msomaji nilishangaa kua eti yeye hawezi kufanya kazi kama izo
nilipoendelea kumdadisi nikakuta kua anaogopa kufanya kazi iyo kwa sababu anaona aibu iliniuma sana kuona kijana
mdogo kama yule anakubali asifanye kazi eti kwa sababu anamuogopa Rafiki au jirani atamcheka nikamuuliza je huyo
mtu unae muogopa anakusaidia kitu chochote katika hali hii uliyo nayo cha kushangaza anae muogopa hamsaidii chochote

Ndugu msomaji kila kitu ni wewe mwenyewe kama utaithamini na kuiheshim kazi yako au biashara yako naamini watu wote
wataithamini na kuiheshim kama utaidharau basi kila mtu atadharau shughuli yako.




Ngaja nikupe mfano mdogo wa kijana Sibusiso alitokea katika familia ya kawaida (yaani sio masikini wala matajiri)
alipomaliza elimu yake ya secondary hakubahatika kuendelea na masomo alikua mtaani mpaka siku moja akaamua aanzishe
kitu kitakacho weza kumuingizia angalau fedha kidogo basi alianza kwa kuzoa taka taka katika majumba ya watu na kila nyumba
alichaji 1000 kulingana na wingi wa taka hizo.watu wengi walimcheka wengine walimdharau kwa kazi yake iyo ndugu msomaji hata
mimi nilishangaa kwa nini Sibusiso kaamua kufanya kazi iyo sababu alikua kijana mtanashati msafi na muadilifu.kadri siku zilivyoenda
na Sibusiso alizidi kuendelea alianza kwa kubeba akanunua mkokoteni akaongeza wa pili akaendelea kuongeza mikokoteni na na kuwaajiri
na watu wengine nilichojifunza kwa Sibusiso aliiependa kazi yake aliifanya kwa malengo aliendelea kuwa msafi wa mwili na nguo zake
ingawa alikua mzoa taka alipata umaarufu mkubwa kwa kazi yake iyo alifanikiwa kupata Ofisi aliendelea kuongeza wafanyakazi mpaka
sasa Sibusiso ni Tajiri mkubwa mwenye kampuni ya kuzoa taka taka na kutunza mazingira ana magari ya kisasa ya uzoaji taka na kutengeneza mbolea
yule yule Sibusiso mzoa taka sasa ni milionea kwa kazi yake iyo iyo ya taka taka je angetuonea aibu majirani angepata mafanikio aliyo nayo

Ndugu msomaji usipoteze wakati na muda wako kwa sababu ya aibu au fulani atanicheka ondoa aibu leo fanya unachofikiria
kitaweza kukuletea maendeleo makubwa kwani matajiri wangapi wameanzia kwa kuuza karanga au pipi bara baran kinachohitajika ni malengo
peke
Mfano una shilingi elfu 10 huna kazi wala biashara basi jaribu kuunda hata kibiashara kidogo ili ile elfu 10 iendelee kuwepo na
kukuletea faida unaweza nunua samaki 6000 mafuta ya kula 200 na kuni au mkaa 1000 viungo na mahitaji madodo madogo 1000
ukakaanga samaki na kuanza kuuza kama utakuwa na malengo ya kuendelea basi unaweza ukashangaa ile biashara ndogo ikakupelekea
kufungua nyingine na nyingine
Biashara ya samaki nimetolea mfano tu ila najua ndugu yangu msomaji una miradi zaidi ya huo ila tu unaona aibu kuanzisha kisha unamuogopa
fulani au fulani atanicheka usirudi nyuma anza na kidogo kikubwa kinakuja muangalie Sibusiso songa mbele Muombe Mungu panga malengo
usikate tamaa mafanikio yanakuja