RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MH. DKT AUGUSTINO LYATONGA MREMA AMSHUKURU BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KWA KUWATOA WAFUNGWA 78 GEREZANI NA AMWITA "MAMA MWENYE HERI NA AMFANANISHA NA MT.THERESA WA INDIA

Mh. Dkt. Augustino Mrema siku ya Alhamisi 15.09.2016 alimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kitendo alichowatoa wafungwa gerezani 78 akishirikiana na waamini wa kanisa la Mlima wa Moto kuwalipia faini ya mil.25. Alisema alichokifanya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ni wokovu wa kuwakomboa watu wanaoteseka magerezani kwasababu ya kukosa fedha za kulipa faini na pia amesababisha kuwaunganisha upya na familia zao na hivyo watawawezesha watoto wao kwenda shule. 


Kitendo hicho kimepunguza msongamano wa wafungwa gerezani na kuokoa fedha za serikali ambazo zilikuwa zinatumika kuwalisha wafungwa wao. Aliongeza kusema kitendo alichokifanya ni kitendo kitakatifu ambacho hakijawahi kufanywa na mtu yeyote kwenye historia ya nchi yetu kwahiyo anastahiri kuitwa "MTAKATIFU MWENYE HERI" sawa na mtakatifu Theresa waindia ambaye alitumia maisha yake yote kuwasaidia watu maskini na wasiojiweza.

Kwaniaba ya Bodi ya Parole ya Taifa na serekali alimshukuru tena na kumuomba aendelee na moyo huo wa kuwakomboa wafungwa wanaoteseka kwa sababu ya kukosa fedha. Alisema kuna wafungwa wanaopaswa kutoka magerezani na kumaliza vifungo vyao nje kwa mujibu wa sheria ya "PAROLE" lakini wanashindwa kutolewa magerezani kwasababu hakuna fedha za kukamilisha mchakato wa "PAROLE", KWANI MFUNGWA ILI AWEZE KUTOLEWA NI MAAFISA WA PAROLE WAFUATILIE KWENDA KUCHUKUA NAKALA YA HUKUMU KWENYE MAHAKAMA ILIYO MUHUKUMU NA WAENDE KUONANA NA UONGOZI WA KIJIJI AU MTAA AMBAKO MFUNGWA ATAENDA KUISHI ANAPOTOKA GEREZANI, PAMOJA NA KUONANA NA FAMILIA YAKE NA PIA KUONANA NA WATU ALIOWAKOSEA.

Pia aliongeza kusema kuna baadhi ya wafungwa ambao ndugu zao wanaouwezo wakutoa fedha za kukamilisha mchakato huo, au ndio wanaotoka. Lakini waliowengi hawana fedha hiyo wanaendelea kusota magerezani. 

Mh. Dkt. Augustino Mrema kwa niaba ya Bodi ya Parole Taifa alimuomba Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aisaidie Bodi ya Parole Taifa iweze kukamilisha kazi hiyo ili kuwawezesha wafungwa wote wenye sifa ya kutoka magerezani kwa mujibu wa sheria ya Parole waweze kutolewa na kuungana na familia zao.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa dini zote wamuunge mkono Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuwalipia faini wafungwa waliofungwa kwa kukosa fedha za kuwalipia faini. Na pia kuisaidia Bodi ya Parole Taifa ili iweze kutekeleza mchakato wakuwatoa wafungwa wote wanaostahiri kwa i kwa mujibu wa sheria ya Parole kama ilivyoelezwa awali.

Pia alimuomba Bishop Dr. Gertrude Rwakatare awe mratibu wa zoezi hili la kukusanya michango kwasababu yeye ndiye muunzilishi wa kampeni ya "KUWAKOMBOA WAFUNGWA KUTOKA MAGEREZANI ".

Hayo ndiyo aliyozungumza Mh. Dkt. Augustino Mrema mbele ya wachungaji, wazee wa kanisa, wainjilisti wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" pamoja na waandishi wa habari.

Tembelea www.mountainofiretanzania.blogspot.com