RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RAIS MAGUFULI AANZA KUWASHUGHULIKIA WANAOHUJUMU MISAADA KAGERA


September 27 2016 taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada wa Milioni 545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda. 

Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo. Hata hivyo Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya “Kamati Maafa Kagera” ambayo imetangazwa na Serikali.