RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RIPOTI: ASILIMIA 90 YA WATU DUNIANI HUVUTA HEWA CHAFU_ WHO.

Leo September 27, 2016 imetoka Ripoti ya Shirika la afya duniani WHO, ikieleza kuwa watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu duniani kote kila siku. WHO sasa wamezitaka serikali za nchi zote duniani kuweka mikakati ya kupambana na uchafuzi wa hewa. Kutokana na hali hiyo kuendelea kwenye maisha ya kila siku, imesababisha binadamu kuambukizwa magonjwa mbalimbali na hivyo zaidi ya watu Milioni 6 kupoteza maisha.


Kwa mujibu wa Maria Neira ambaye ni Mkuu wa kitengo cha WHO kinachoshughulikia afya za wananchi na Mazingira amesema, watu wanaoishi mijini ndio wanaothiriwa zaidi na kuwepo kwa hewa chafu.

Hata hivyo, watalaam wa WHO wanasema hali hii ni mbaya zaidi vijijini kinyume na inavyodhaniwa na wengi. Aidha, ripoti hii inaeleza kuwa nchi masikini duniani ndizo zinazoathiriwa zaidi zikilinganishwa na zile zilizoendelea.

Kutokana na hali hii, Ripoti iliyotolewa na WHO baada ya kufanya utafiti katika maeneo elfu tatu kote duniani. inasema afya ya binadamu ipo hatarini huku mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia yakitajwa kuathiriwa zaidi hasa nchi za China, Malaysia na Vietnam.