MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SAKATA LA JARIBIO LA KUMPINDUA RAIS WA UTURUKI LACHUKUA SURA MPYA

Waziri Mkuu wa Uturuki, amesema zaidi ya watu 40,000 wanashikiliwa na Polisi wakihusishwa na jaribio la kutaka kuipindua Serikali ya rais wa nchi hiyo, Erdogan.

Katika hotuba yake ya moja kwa moja katika Televisheni, Binali Yildirim pia alisema takriban wafanyakazi wa sekta ya Umma 80,000 wamefutwa kazi wakiwemo wanajeshi, Polisi na watumishi wa Umma.

Maelfu ya Taasisi yameshukiwa kuwa na mahusiano na Kiongozi wa kidini, Fethullah Gulen zimefungwa.

Serikali ya Uturuki imemshutumu Gulen, ambaye anaishi uhamishoni nchini Marekani kwa kusuka mipango ya mapinduzi .

Awali, Serikali ya Uturuki ilisema itawaachia huru watu 30,000 ili kupunguza mrundikano kwenye magereza.