MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KWA WAATHIRIKA WA AJALI MKOANI NJOMBE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force iliyotokea  Sept 19, 2016 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Lilombwi, kata ya Kifanya mkoani Njombe.

Ambapo watu 12 wamepoteza maisha na wengine 28 kujeruhiwa, basi hilo limepinduka katika kona ya barabara wakati likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Songea mkoani Ruvuma.

‘Ndugu Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi naomba unifikishie pole nyingi kwa wote waliopatwa na msiba, wamepoteza wapendwa wao, wamepoteza watu waliowategemea’

‘Sote tuwaombee wote waliofikwa na msiba wawe na moyo wa subira, uvumilivu na pia tuwaombee Marehemu wote wapumzishwa mahali pema peponi Amina’- Rais Magufuli