RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UINGEREZA NAYO YAGUSWA NA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA


Wakati taasisi, mashirika, nchi mbalimbali na watu binafsi wakiguswa kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera, Leo September 28 2016 Uingereza imeingia kwenye list ya nchi ambazo zimetoa msaada kwa waathirika ambapo imetoa Bilioni 6.

Mchango wa fedha hizo umewasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke, Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho.

Balozi Sarah Catherine Cooke amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na kutoa mchango wa fedha hizo Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May anatoa pole kwa Serikali ya Tanzania na kwa familia zote zilizopatwa na madhara ya tetemeko hilo na kwamba Uingereza imeona ishirikiane na Tanzania katika kukabiliana na madhara hayo.

‘Uingereza imeguswa sana na maafa yaliyowakumba wananchi kufuatia tetemeko lililotokea Kagera, tunapenda kuona wananchi wanasaidiwa na wanafunzi wanaendelea na masomo”-Balozi Sarah Catherine Cooke’.

‘Balozi Sarah Catherine Cooke naomba unifikishie shukrani zangu za dhati kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na umueleze kuwa kwa niaba ya watanzania hususani waliopatwa na madhara ya tetemeko la ardhi tumeguswa sana na moyo wake wa upendo kwetu’-Rais Magufuli.