SHILO TANZANIA

SHILO TANZANIA

SHILO TANZANIA 2017

UMMY MWALIMU ATOA ONYO KWA WAZAZI WA WANAFUNZI WANAOMALIZA STD VII


Mhe. Ummy Ally Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Serikali ya Awamu ya Tano, ametoa onyo kwa wazazi wa wanafunzi wa darasa la saba wanaofanya mitihani yao ya taifa leo. Ummy ametoa onyo hilo kupitia akaunti yake ya Facebook ambapo pia alichukua muda wake kuwatakia kheli wanafunzi hao wanaofanya mitihani ya kumaliza elimu yao ya msingi;

Hivi ndivyo alivyoandika;  

Nawatakia kila la kheri watoto wote wanaofanya Mitihani ya kumaliza darasa la saba.
Ni matumaini yetu kuwa watoto wote watafaulu vizuri na hivyo kupata fursa ya kuendelea na Elimu ya Sekondari.

Pia wakati watoto hawa watakapokuwa wanasubiri matokeo yao, ni matarajio yangu na Matarajio ya Serikali kuwa wazazi/walezi watawapa fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yatakayosaidia kuimarisha malezi na makuzi yao pamoja na kujiandaa na masomo ya Sekondari.
Na kwa upande wa wasichana, nitoe #Onyo kwa Wazazi/Walezi kutowaozesha Watoto hawa wakati wanaposubiri majibu ya Mitihani yao. Ndoa kwa wasichana sio njia muafaka ya kutatua changamoto za kifedha za wazazi/walezi.

Bali Elimu. Hivyo ni muhimu kwa kila Mzazi/Mlezi kuhakikisha mtoto wake wa kike na wa kiume anaendelea na Elimu ya Sekondari. #ElimuNdioMkomboziWaKweliKwaWasichana

SHILOH TANZANIA 2017

SHILOH TANZANIA 2017