RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: BAADA YA DARAJA LA KIGAMBONI, DARAJA LINGINE KUJENGWA DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya Mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young, Ikulu Jijini Dar es Salaam na baada ya mazungumzo hayo Rais Magufuli amepokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salender litakalojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi huyo.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani na unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na daraja hilo litasaidia kupunguza adha ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Ujenzi wa Daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo Agha Khan kupitia baharini Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza Mwezi Juni Mwakani baada ya Serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa fedha za ujenzi kutoka benki ya Exim ya Korea. 

>>>’Mchakato wa kulijenga hili daraja la Salender unaendelea vizuri kwa sababu hivi sasa kampuni ya Kikorea ambayo inafanya usanifu ipo kwenye hatua za mwisho na zabuni zinategemewa kutangazwa mwezi wa tatu Mwaka kesho na zitakwenda haraka, kwa hiyo mambo yakienda vizuri ujenzi unaweza kuanza mwezi wa sita, bahati nzuri fedha zote zipo na zimeshatolewa na Benki ya Exim ya Korea’:- Rais Magufuli.