MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

VIDEO: HIKI NDICHO KIZAZI CHA BAHATI BUKUKU,CHRISTINA SHUSHO,UPENDO NKONE,ROSE MUHANDO,JOHN LISU.Siku zinavyo zidi kwenda maneno shawishi kupitia Uncle Jimmy na Samuel Sasali yameanza kuonekana machoni pawatu. Leo tunaona mabadiliko makubwa katika utengenezaji wa video za muziki wa Gospel Tanzania. Ukiliacha hilo la video za muziki wa Gospel leo nataka nikuonyeshe kizazi kinachokuja kuchukua nafasi ya Christina Shusho,Upendo Nkone,Bahati Bukuku,Boni Mwaitege,John Lisu,Rose Muhando,Upendo Kilahiro na wengine wengi. Niwazi kabisa waimbaji hawa wakubwa wenye majina yao kwa sehemu kubwa…niruditena kwa sehemu kubwa wamechonga barabara katika muziki huu hivyo tunatambua mchango wao,ila kanuni ya Mungu uinua mtu mwingine kama Biblia isemavyo. Sasa basi kwa hisani ya Unclejimmytz na Jt TV angalia vijana hawa Kumi na Tano kisha niambie unaona nini baada ya miaka 10 katika muziki wa Injili Tanzania.
Utapenda kuwaona tena vijana hawa wa Gospel Star Search?….Siku ya Kesho katika ukumbi wa MIRADO ulipo sinza vijana hawa watakua wakifanya LIVE kwenye fainali za Gospel Star Search 2016. Kumbuka ni Sinza Siku ya Kesho kuanzia saa tisa alasili hadi saa kumi na mbili jioni. Kiingilio Sh 20000 Kwa VIP na Kawaida Sh 10000. Karibu sanaaa!!