RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAZEE WAHOFIA CHADEMA KUHUJUMIWA

BARAZA la Wazee la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limesema lina hofu ya kuhujumiwa chama chao kupitia kwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kuundiwa njama za kukifuta chama hicho kwenye orodha ya vyama vya siasa.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Baraza la Wazee Taifa wa Chadema, Roderick Lutembeka, amesema pamoja na juhudi kubwa wanazozifanya kutatua mgogoro wa kisiasa, wamepata taarifa za kuwepo kwa njama hizo zinazopikwa dhidi ya Chadema kupitia baraza la vyama vya siasa.

“Ni vyema msajili wa vyama vya siasa akawa wazi kwa Watanzania kwani Baraza la Vyama vya Siasa lililo chini yake limekuwa likiaandaa na kuahirisha vikao vya kukutana na vyama vyote vya siasa pasipo kututaarifu.

“Mfano Agosti 29-30, ilikuwa baraza likae lakini likaahirisha hadi Septemba 3-4 napo pia wakaahirisha tena bila sisi kupewa taarifa yoyote,” alisema Lutembeka.



Katibu Mkuu Baraza la Wazee la Chadema, Roderick Lutembeka akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), pembeni yake ni mjumbe wa baraza hilo, Alfred Ntupwa.


Lutembeka akiendelea kusoma taarifa yake.

Wanahabari wakichukua tukio hilo