RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ZITTO KABWE ATAKA WALEMAVU WATHAMINIWE, WAWEZESHWE

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati) akizungumza jambo katika hafla hiyo.
zitto-kabwe-3-001Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, Aneth Gerano (kulia) akizungmza jambo mbele ya mgeni rasmi.
zitto-kabwe-4-001Zitto akiangalia baadhi ya bidhaa zilizozalishwa na watu wenye ulemavu katika uzinduzi huo wa Wiki ya Viziwi katika viwanja vya Biafra Kinondoni Dar.
zitto-kabwe-5-001Mtaalam wa teknolojia, habari na mawasiliano (TEHAMA) ambaye ni bubu (kushoto) akimweleza Zitto namna wanavyokabiliwa na changamoto. Aliye na maiki (kulia) ni mkalimani.zitto-kabwe-6-001Baadhi ya wasiosikia waliofika katika uzinduzi huo.zitto-kabwe-1-001Zitto (katikati) akiwa katika picha na watu wenye ulemavu.
KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema walemavu ni watu muhimu na wanaopaswa kuthaminiwa katika jamii kwani wakiwezeshwa wanaweza kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa taifa.
Ameyasema hayo leo katika viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Wiki ya Viziwi Kimataifa inayoanza leo hadi Septemba 30 mwaka huu.

Katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, Aneth Gerano, alisema wiki hiyo huonesha bidhaa mbalimbali zinazofanywa na walemavu kupitia taasisi zao na kuieleza serikali changamoto zinazowakumba.

Gerano alimkabidhi Zitto hotuba yake ili kuzifanyia kazi changamoto walizozisema walemavu wakati atakapokuwa bungeni.

Naye Zitto baada ya hotuba hiyo alisema hana sababu ya kuhitaji kujua watu wenye ulemavu ni watu wa aina gani kwani yeye amelelewa na mama yake mlemavu enzi za uhai wake ambapo anazijua sababu mbalimbali wanazokabiliwa nazo.

Alisema yeye kama mbunge anapaswa kupaza sauti za watu walemavu ili zisikike kupitia nguvu za wabunge na serikali kuzifanyia kazi. Shughuli za wiki hii ya watu wasiosikia, zinaenda sambamba kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu mbalimbali nchini inayotarajiwa kufanyika Desemba 3 mwaka huu.