RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

16.10.2016: KWAYA YA MLIMA WA MOTO YAFANYIKA BARAKA SIKU YA JUMAPILI


Hakika siku ya Jumapili 16.10.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ilikuwa ni siku ya Baraka sana kwa wale waliobahatika kufika na kuabudu pale. Kwaya za Mlima wa Moto Mikocheni "B", Happy Kwaya na Joybringers Kwaya zilitubariki sana kwa nyimbo zao zenye upako wa aina yake. Hakika Mungu anawatumia watumishi wake kwa kazi yake. 

Watu wengi sana wamekuwa wakibarikiwa sana na waimbaji hawa kutokana na nyimbo zao kuwa na ule ujumbe mzito unaogusa maisha ya watu na pia jinsi wanavyocheza mbele za Mungu.

Jumapili hii ya ISHARA na MIUJIZA watakuwepo nyumbani mwa Bwana kwa kazi moja tu ya kumsifu na kumuimbia Mungu wetu wakishirikiana na Martha Mwaipaja. Itakuwa ni siku ya baraka kwako na kwangu pia. Tunakualika wewe na rafiki zako ili tupokee baraka za Mungu pamoja. Ibada itaanza saa 3 asubuhi mpka saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo ch mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenya mataa barabara ya kuelekea kiwanda cha Coca Cola. Utasikia watumishi wa Mungu wakisema, "Kwa Mama Rwakatare" Ingia humo.

 Victor Aron Mtangazaji wa Praise Power akiwa aki lead