RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

16.10.2016: MAPEPO, MAJINI, NGUVU ZA GIZA ZA SALENDA NA KUTOKOMEA HUKU WATOTO WA MUNGU WAKIACHW HURU NA MATESO SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Bwana ni Bwana wa wote, hachagui dini, kabila, rangi, kipato, uwezo wa mtu, bali yeye ni Bwana wa wenye haki. Tumeona akifanya mambo mengi sana katika huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa ishara, miujiza na uponyaji kupitia kinywa cha mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wachungaji wa kanisa hili. Watu wengi wanakombolewa na wanawekwa huru kwa jina la Yesu. Mungu anatupenda kwasababu tunampenda na ndio maana anazidi kutubariki na kutulinda na mabaya kila kuitwapo leo.

Mch. Noah Lukumay akisambaratisha kazi za shetani

Siku ya Jumapili 16.10.2016 katika kanisa hili aliweza kufanya mambo makubwa sana na kusababisha watu kukuna vichwa jinsi alivyokuwa akijidhihirisha kupitia watumishi wake wa Mlima wa Moto Mikocheni “B”.
Mch. Elizabeth akimuombea bibi

Mch. Noah Lukumay, Mch. Francis Machichi, Mch. Elizabeth, Mch. Prisca, Mch. Otieno, Mch. Mama Mgetha na wainjilisti wa kanisa hili, waliweza kushambulia mapepo, majini, wachawi na nguvu zote za giza kwa kuwaombea watu katika kipindi cha maombezi na uponyaji. 
Watu wengi walitokwa na mapepo na nguvu za giza huku wakipiga kelele na wengine kuangushwa chini kwa nguvu za Mungu mara tu watumishi wa Mungu walivyoweza kutamka maneno ya mamlaka ya kuwaachilia watoto wa Mungu kuwa huru.

Ibada hii iliwashangaza sana watu waliweza kuhudhuria jinsi Mungu alivyoonekana kwa njia ya ajabu sana. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu alivyoyafanya Jumapili kupitia watumishi wake. Tunakushuru na wewe uliyefika na kuambukizwa nguvu za Mungu ndani yako ambazo zinafanya kazi mpaka sana, na ndio maana bado unaishi.
Mch. Mama Mgeta akimuombea mtu mwenye mapepo

Tunakukaribisha sana katika ibada ya Jumapili hii ya ISHARA NA MIUJIZA katika kanisa hiili la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Ibada itaanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 8 mchana. Katika ibada hii kutakuwa na mwimbajiwa nyimbo za Injili Martha Mwaipaja, Joybringers Kwaya na Happy kwaya za Mlima wa Moto Mikocheni “B”. 

Yawezekana unapitia mateso Fulani, Jumapili hii kuna jibu lako, unatakiwa kuja ukiwa na IMANI kuwa utaondoka na muujiza kwako kwa jina la Yesu Kristo. Jisafishe kiroho kwa kutubu na kuomba ili siku hiyo iwe ni siku ya kupokea Baraka za Bwana katika maisha yako.

Mch. Otieno akimuombea mtu mwenye pepo






 Godfrey katika kazi ya Bwana