MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.10.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AMSIFU MARTHA MWAIPAJA KWA UIMBAJI WAKE NA KUJIHESHIMU


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 23.10.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kumshukuru na kumpongeza mwimbaji wa nyimbo za Injili Martha Mwaipaja kwa kuimba katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, alisema, ”Bwana apewe sifa, Tumemuona Martha Mwaipaja akiwa msichana mdogo kabisa, mwembamba akiimba, mara ya mwisho nakumbuka aliimba kwenye harusi mwanangu Tibe.
 Nakumbuka aliimba wimbo akiwa na mimba kubwa ya mtoto wa kiume. Namshukuru Mungu kwa jili yake anachonibariki Martha ni kwamba hajaacha ule uimbaji wake, anaimba kama shahiri, sasa lile shairi linapenya mpaka ndani ya moyo na ndio maana machozi yanabubujika anapo imba. Sasa mimi niliyeokoka naguswa namna hii, Je yule ambaye hajaokoka? 
Ujumbe huu unagusa na wale wanaopita kwenye matatizo. Usiku nilikuwa nampigia mama Mshombozi, tukawa tunaongea, akaniambia, “Mama kesho nijaribu kuja kanisani, nimeona bora niache kazi niende madhabahuni nikamrejee Mungu”.
 Akasema, “Hivi kweli ananiona, ananisikia?” Akasema, “Mbona Mungu anaponya, anaokoa, kwanini mimi nimeokoka bado mateso yapo?” Lakini alivyokuwa anaimba Martha, nikasema “Huu ndio ujumbe wa mama Mshobozi”. Nyimbo hizi ni mahubiri tosha, zinatia moyo na zinabariki. Martha endelea kuimba tena na tena ukimtukuza Mungu. Hakika utafanyika Baraka kwa ya mume wako na hata kwa huduma hii.Mungu akubariki sana Martha Mwaipaja.xx