MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.10.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE NA MCH. NOAH LUKUMAY WALIVYOONGOZA KIPINDI CHA MAOMBEZI KATIKA IBADA YA ISHARA NA MIUJIZA SIKU YA JUMAPILI

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikina na Mch. Noah Lukumay wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kuwaombea watu wenye mahitaji mbalimbali. Watu wengi waliweza kufunguliwa na kupokea miujiza yao. Kumbuka ibada hii ilikuwa ni ibada ya Ishara na Miujiza, kwahiyo watu walipokea kile ambacho walikuwa wakikihitaji katika maisha yao. Ilikuwa ni ibada ya baraka sana kwa wale waliobahatika kufika katika ibada hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kuna watu waliweza kutokwa na mapepo, majini, wachawi waliwaachilia kwa damu ya Yesu. Pia waliweza kushiriki Meza ya Bwana kwa kula mwili wa Kristo na kunywa damu ya Yesu.

Mch. Noah Lukumay
Hakika tunajivunia sana wokovu huu tuliopata kwa neema tu ya Mungu. Tunakualika wewe ambaye hujabahatika kufika katika kanisa hili ili uweze kupokea hitaji lake. Mungu yupo karibu na wewe usikate tamaa. Mungu wetu anafanya mambo yake kwa UKUBWA pale tu utakapomkubali na kumtumikia. Rafiki yangu nakusihi sasa uanze maisha ya kumtumikia Mungu kwa hujui kesho yako itakuwaje. 
Kuna faida nyingi sana ukiishi maisha ya kumpendeza Mungu. Tunatambua kuna changamoto za kimaisha ambazo zinakusababisha hata kumsahau Mungu wako lakini tambua ipo siku utatafuta wokovu na hautaupata. Mpokee Bwana kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako sasa. Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. 

Mungu akusaidia ufike ukiwa umeongozana na mwenzako ili na yeye afurahie Mungu unayemtumikia wa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mungu akubariki sana. Unaweza kutembelea blogu yetu, www.mountainoffiretanzania.blogspot.com kujua mengi kuhusu huduma hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"