23.10.2016: KWAYA ZA MLIMA WA MOTO ZAKONGA MIOYO YA WATU SIKU YA JUMAPILI

Happy Kwaya na Joybringer Kwaya za kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" zimefanyika baraka kwa watu wengi sana kutokana na uimbaji wao na hasa ule ujumbe wanaoutoa kwa jamii. Siku ya Jumapili 23.210.2016 waliweza kumtukuza Mungu katika ibada ya Isahara na Miujiza  iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Hakika waimbaji hawa walifanya vizuri sana na watu kujikuta wanainuka katika viti vyao na kwenda kuwapongeza. Tuna kila sababu ya kuwapongeza na tuzidi kuwaombea. Jumapili hii watakuwepo nyumbani mwa Bwana, kwahiyo tunakukaribisha sana na ibada itaanza saa 3 asubuhi mpaka saa 8 mchana. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa kanisa hili wamejipanga kukuombea na kukutamkia maneno ya baraka kwako. Mungu akubariki sana.