RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.09.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE TANGAZO LA KIINGEREZA


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 25.09. 2016 aliweza kutangaza rasmi juu ya masomo yatakayokuwa yakifundishwa chini ya huduma ya kanisa la Mlima wa Moto Tanzania, alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu apewe sifa. Jamani kuna kozi ya Kiingereza na Kifaransa na Kompyuta itakayokuwa ikitolewa na huduma yetu ya Mlima wa Moto Tanzania. Kila somo utalipia sh.10,000 kwa mwezi mzima na utaweza kuongea Kiingereza ndani ya mwezi mmoja. Unajua sasa hivi wanakuja wawekezaji wengi ambao hawajui Kiswahili na lugha wanayotumia ni Kiingereza na Kifaransa tu pia kumbuka tunaingia Afrika Mashariki ambayo inahitaji watu waongee Kiingereza au Kifaransa, na tunasikia kuwa Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda wanaongea Kiingereza kwahiyo Kiingereza ni kitu muhimu sana kukijua. Gharama yake TSh. 10,000 kwa mwezi mzima. Jamani hakuna tena kozi rahisi na nyepesi kama hiyo. Halafu kuna Kifaransa, kwa mfano Waburundi wameingia Afrika Mashariki, Wakongo wapo mbioni kujiunga, pia Rwanda wamejiunga. Hawa watu wakijiunga ni kwamba tutakuwa tunauwezo kushirikiana nao kibiashara, kuhubiri injili, kwahiyo ni vizuri angalau kujua cha kuombea hata maji. Unakaa kwenye mgahawa unashindwa kuongea Kiingnereza au Kifaranza unabaki kuonyesha kwa vitendo pale unapohitaji kitu usaidiwe, ni aibu. Nafikiri ni bei rahisi na kila mtu anaiweza kulipia na kujifunza. Wahusika watakueleza kwa kina jinsi ya kujiunga. Kwa kozi zote tatu, kuchukua fomu unainunua kwa sh. 10,000 unaijaza alafu utachagua somo moja au mawili au yote matatu kwa Tsh. 10,000 kwa kila kozi moja.Hakika naamini sauti hii imepata kibali masikioni mwenu.” 
Unaweza kumpigia simu JONATHAN KIBONA +255 653 592 322 kama utahitaji kujua mengi juu ya OFA hii. Mungu awabariki sana.