RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.09.2016: MCH. NOAH LUKUMAY: WATU WANWEZA KUKUONA WEWE SI KITU LAKINI WEWE USIWATAZAME WAO MUANGALIE MUNGU NA USIKATE TAMAA.

Watu wanaweza wasikuone wewe ni kitu lakini wewe usiwatazame kwani mahali unapoelekea ni mahali pa kishindo kikubwa, unaenda kusababisha mazingira mazito, unaweza ukadharaulika lakini usiogope maana safari yako siyo safari ya wale wanao kupinga bali ni safari ya yule aliyeanzisha ambaye ni Mungu mwenyewe. Upepo unaovuma hauwezi ukauzuia, kila mtu anajua ya kuwa upepo hauzuiliki? Kama upepo hauzuiliki na chochote ni sawa na mtu wa Imani hazuiliki kwa lolote, hata kama amechelewa hataishia pale alipo wala atafia alipo bali anaelekea mahali pa kuwashanganya wengi. Watu wanaokusimanga, waache wakusimange sana, ili watakapokifika kule mbele unakoelekea watakushangaa na kutengeneza habari nyingine juu yako wakiseme, “huyu ni nani mbona alikuwa haeleweki lakini sasa amekuwa mtu wa maana sana. Ninachotaka kuambia ni kwamba baada ya muda watakuelewa wewe ni nani katika dunia hii. 
Mch. Noah Lukumay

Wakati Obama akigombea kinyang’anyilo cha uchaguzi wa Rais nchini Marekani alikuwa hajulikani kabisa maana angejulikana kuwa Rais wa Marekani yamkini kila mtu angeomba nafasi yake, yamkini kila mtu angekuwa karibu yake, kila mtu angeweza kuomba apige picha naye, yamkini watu wangeomba wapate “Lunch” naye, lakini Mungu akayaficha hayo. Inawewzekana Rais Obama alikuwa anajiuliza “hivi kweli siku moja nitakuwa Rais wa Marekani na dunia itatambua.

Kumbuka ya kuwa roho iliyopo ndani ya mtu ndio inayotawala. Obama alipoingia katika mchakato wa kuwainia urais Marekani, wakasema, “Sasa wewe Mtu mweusi ni moja ya watu ambao hawatakiwagi kwenye hii nchi ya Marekani kushika madaraka makubwa inakuaje leo unagombea urais Marekani?”, Akasema, “Bwana siingii kwa sababu mimi ni mtu mweusi ila nimeingia kwa sababu nina Urais, nina cheo ndani yangu, nina nafasi ndani yangu, siyo kwa sababu watu wengine wanashindania furaha ipo ndani yangu”. Kila yale unayoamini yakili ila usikili yale unayosiki watu wanasema juu yako na kukukatisha tamaa. Watu walimwambia Obama, “hutaweza”, nafsi mwake akasema, “mimi sitaingia kwa neema ninaingia kwa Roho”. 

Kuna watu hawatainuliwa kwa sababu ya pesa, kuna watu hawataonekana kwa sababu ya pesa bali kwa Roho ya Mungu iliyopo ndani yake itasababisha waonekane, itasababisha wewe uchaguliwe, utaonekana kwa sababu ndani yako kuna kitu unachotaka. Wakati Bathromayo akipiga kelele, Yesu hakuwa na haja na yeye lakini alitaka apige kelele zake na wanafunzi wake walimwambia, “nyamaza” na yeye hakunyamaza. Na wewe usinyamaze hata ukisikia watu wanakusengenya usianze kurudi nyuma kwasababu watu wanaongea usianze kurudi nyuma kwa sababu watu wanakukatisha tamaa endelea kusonga mbele palepale kwa sababu baada ya kusengenywa watatengeneza habari nyingine kwa ajili yako, usikate tamaa kwa maneno ya watu.