RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.09.2016: MCH. OTIENO: IMANI INAMFANYA MTU KUWA MTAKATIFU NA AKIKILI ANAPATA NGUVU YA KIMUNGU NDANI YAKE

Imani hiyo inafanya mtu kukili na katika kukili kuna nguvu, soma Mathayo 16,19 na 18 . Imani ndiyo inamfanya mtu kuwa mtakatifu. Utakatifu ambao unamuongoza mtu na kutotendatenda dhambi au kufanya mambo machafu, imani inahitaji utakatifu ndiyo hii inatutofautisha na watu wa mataifa. Ukiniambia wewe umeokoka na ni tajiri umepata mali, lakini hata yule wa mataifa ana magari zaidi yako, kwahiyo ni lazima tuwe tofauti na wao kwasababu ya utakatifu wetu, tutembee na maisha ya utakatifu. Huwezi kuwa na maisha ya utakatifu kama hauna imani yenye matendo, imani ambayo hauwezi ukamwabudu mtu kwa sababu ya fedha zake, ambazo zinaweza kukuingiza kwenye mambo machafu. Kutokana na njaa unasema, “Hata kama sina pesa siwezi nikatenda dhambi, nataka nitembee maisha ya utakatifua”. Hivi sasa utakatifu umepotea kwahiyo lazima tuutafute, watu wanatafuta miujiza lakini hawana utakatifu. Mathayo 7:21-22,23 anasema, “Kwa jina langu utatoa mapepo, kwa jina langu utatoa unabii, kwa jina langu utaombea wagonjwa, lakini wataambiwa tokeni kwangu nyie watenda dhambi”. Unadhani ukitoa mapepo na kutabili ndio tiketi ya utakatifu wa kwenda mbinguni? Unaweza ukaombea mapepo yakatoka, unaweza toa Unabii lakini siku ya mwisho utaambiwa, “Tokeni kwangu nyie watenda dhambi siwajui”, Usibabaike na kutoa mapepo hata ukiombea wagonjwa wahawezi kutembea zigizaga, lazima uwe na utakatifu, lazima udumu nyumbani mwa Bwana. Soma, Wakolosai 3:8-10 , 1Petro 15-16, 2Wakoriso 6:14-18, Daniel1:5-9,17-20 utaona ambapo wakati Danieli alikata kula chakula cha unajisi walichokuwa wamepewa na Mfalme, wengi wanakula chakula cha unajisi siku ya leo. Ujumbe huu ni sehemu ya mahubiri ya Mch. Otieno siku ya J’pili 25. 09.201