25.09.2016: MCH. OTIENO: MAMBO HAYAKUENDEI SAWA KWASABABU HUOMBI HUNA IMANI YA MATENDO.


Biblia inasema, “Daniel nae alikuwa kwenye maombi, Musa nae alikuwa kwenye maombi, alipo panda mlimani aliposhuka sura yake iling’aa watu wakaogopa hata kumtazama usoni, watu wakapotea”. Ninaomba wiki hii, mwezi huu wa imani Mungu akuandalie maombi ya kwako, hata kama haijatangazwa madhabahuni kuwa uanze maombi, wewe anza maombi. Vitu vimesimama, mateso yanaingia kwenye nyumba, watoto wanaugua ugua, unaota ndoto mbaya kwa sababu huombi. Anza maombi ya Utakatifu utaona Mungu akishuka akigusa maisha yako. Hauwezi kuingizwa kwenye dhambi na wewe ukakubali kwasababu ni mtu wa amombi, Roho ya Bwana itakuongoza. Wewe utakuwa msaada wa kanisa lako.
Huu ni ujumbe mfupi katika somo zima la la Imani kutoka kwa Mch. Otieno siku ya Jumapili 25.09.2016