RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.09.2016: MCH. OTIENO: USIOMBE UKIWA NA SHIDA TU, WAKATI UKIWA NA RAHA HUFANYI MAOMBI - USITEGEE


Ukisoma katika Waefeso 6:18, Luka 18:10-13, na Luka 6: 12, 17-19 inasema, “Siku zile Yesu aliondoka akaenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha katika kumuomba Mungu”. Wengi wanataka kuomba wakiwa na shida, akiwa anafukuzwa na mume wake ndiyo anasema, “Mchungaji niombee” hayo maombi ni ya kwako Mungu haingilii maombi ya shida, Mungu anataka maisha ya maombi, yaani maisha yetu yawe ya maombi siyo wakati wa shida. Biblina inasema, “Yesu akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano mkubwa wa watu waliotoka Uyahudi, wote na Yerusalemu na Pwani ya Tiro na Sidoni waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao”. Je, Yesu alikuwa na deni na mtu au amekopesha mtu au ameingia kwenye dhambi fulani? Watu wengine wakiingia kwenye dhambi ndio wanaomba ili Mungu awasamehe. Ni nani alikwambia maombi hayo Mungu anasikia, utasoma Waebrania 6 ukishaujua utamu wa mbinguni na ukaonja utamu wake na ukatenda dhambi unamrudisha mwana wa Mungu msalabani mara mbili. Na mtu anayetenda dhambi hiyo hatasamehewa, usijidanganye eti, tunatubu, kila tunapo anza tunatubu; eti, najua nitatubu hata nikifanya hivi nitatubu. Hiyo siyo dhambi ya kusamehewa, na mtu mwenye maombi hatendi dhambi ya ovyo ovyo. Yesu hakuwa na matatizo ili aingie kwenye maombi ila maombi yalikuwa kwaajili ya maisha yako. Biblia inasema Yesu alipo shuka kutoka mlimani kuomba aliponya wagonjwa, waliooza, waliokata tamaa, waliolilia uponuyaji, aliwaponya kwa sababu gani aliingia kwenye maombi.