MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

25.09.2016: WATU WAZIDI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NA KUPOKEA UPONYAJI WAO SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Praise and Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika kipindi cha kuabudu na kumtukuza Mungu, watumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay, Mch. Otieno, Mch. Francis Machichi, Mch Elizabeth Ngaiza na wengine wengi siku ya Jumapili 25.06.2016 waliweza kutenga masaa kadhaa katika ibada iliyokuwa ikiendelea mahali hapo na kuweza kuwaombea watu wenye mahitaji mbalimbali.

Katika ibada hiyo hakika Mungu alijithihirisha kuwa Yeye ni mtenda miujiza. Watu waliweza kutokwa na mapepo, majini, mikosi na shida mbalimbali baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu waliojaa nguvu za Mungu. 

Baadhi yao waliweza kushuhudia jinsi Mungu alivyoweza kuwatendea baada ya maombezi. Hii ilikuwa ni ibada iliyojaa nguvu za Mungu kwani watu walionekana kuguswa na ule uwepo uliokuwa umetanda katika kanisa hili baada ya Praise and Worship Team kumaliza kuimba.
Tuachotaka kukuambia ni kwamba kuna nguvu katika maombi. Unapokuwa katika shida na raha usisahau kufanya maombi kwani Mungu anaonekana kwako kupitia maombi. Unapomuomba Mungu uwe umemaanisha na ukiwa na imani kuwa kile unachoomba kinaenda kutimia. 
Maombi yako yatajibiwa kama na wewe utaacha kuwa mtu vuguvugu, sio leo kwa Yesu kesho kwa shetani. Ni lazima kuamua moja na kulifanyia kazi kwa nguvu zote ili mwisho wa siku upokee muujiza wako. Na unapopata muujiza unatakiwa kuongeza kiwango cha maombi.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi yanayoombwa na watoto wake wa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunakushukuru na wewe uliyeweza kufika na kuabudu nasi na ukaacha kazi zako na mihangaiko ya kutafuta pesa ukaona ni vyema kuja nyumbani mwa Bwana.
 Martha Komanya akiongoza kipini cha Kusifu na Kuabudu

Tunaamini Jumapili hii itakuwa ni Jumapili ya kipekee katika maisha yako. Tunakuomba uje ukiwa na ile IMANI ya kuwa Mungu anakwenda kusikia majibu yako na kujibu kulingana na haja ya hitaji lako.

Mungu wetu ni Mungu wa huruma na anajibu kwa walio wake na wanaotii maagizo yake kupitia kitabu chake kitakatifu (Biblia).

Unapokuja Jumapili hii jitahidi kuja na mwenzako ili na yeye aweze kuonja ule utamu wa Yesu uliopo katika kanisa lake Takatifu la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ukifanya hivyo utakuwa umefanya Uinjilisti wa kuwaleta watu kwa Yesu. Wapo watu wengi mtaani kwako wanatamani kuwa na moyo wa kuja kanisani ila wamefungwa na nguvu za giza na wanashindwa kuja kanisani, ila utakapowaambia na kuwasaidia kufika kanisa utakuwa umefanya jambo jema. Mungu akubariki sana na tukutane Jumapili saa 3 asubuhi hapa kanisaniu na zidi kutembelea blogu yetu www.mountainoffiretanzania.blogspot.com

 Kutoka kulia Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mzee Malya na Mch. Otieno Mrs. Pastor Noah Lukumay