RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.10.2016: MCH. NOAH LUKUMAY: KUSHINDA ROHO YA KUKATA TAMAA

Tunatakiwa kuishinda roho ya kukata tama. Roho ya kukata tamaa inatembea kwa kila mtu anayeishi duniani Ukiwa katika dunia hii, roho inakufuata. Ukisoma Luka 1:5-14 inasema, “ Zamani za Herode Mfalme wa Uyahudi palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni jina lake Elisabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. Nao walikuwa hawana watoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili walikuwa wazee sana. Basi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, kama ilivyo desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. Akatokewa na malaika wa Bwana amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukiza. Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule malaika akamwambia, usiogope Zakaria maana dua yajo imesikiwa, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake”.

Mch. Noah Lukumay

Sifa ya huyu mtu alikuwa ni kuhani, ni mcha Mungu, ni mtaua ni mtu ambaye alikuwa anakaa siku zote madhabahuni, anashinda mbele za Bwana. Alipokuwa mbele za Bwana amechoka, lakini maandiko yanasema alikuwa na mke wake ambaye alikuwa ni mmoja wa watoto wa Haruni nae alikuwa hana mtoto. Walikuwa na pesa, walikuwa na Mungu, walikuwa wanawaombea watu wanapata watoto lakini wao walikuwa hawapati watoto, walikuwa wanawaombea watu wanapata miujiza lakini wao miujiza yao haikuonekana. Lakini sifa nyingine walikuwa wazee sana na uzee wao ulieliza kuwa maisha yao yataishia vibaya sana kwa sababu hawakuwa na mtoto, lakini wakati walikuwa wakiendelea katika maisha yao wakiwa na jina la utasa maandiko yanasema siku ya zamu ikafika akaingia mbele za Bwana akiwa anafukiza uvumba, akiwa anapeleka mahitaji ya watu akiwa amebeba mizigo ya watu bali alikuwa anabeba na mzigo wake pia. Maandiko yanasema malaika akatokea akamwambia, “Zakaria usiogope”. Leo mwambie jirani yako “usiogope hata kama wewe una matatizo makubwa kuliko ya Zakaria, hata kama wewe una madeni makubwa kuliko kila mtu anayeishi duniani usiogope, usiogope kwa sababu ya hiyo hali inayokukatisha tama”. 


Watu walimwendea Zakaria wakamwambia, “Inakuwaje nyie mnamuomba Mungu na maombi ya watu yanajibiwa lakini ya kwako hayajibiwi?” Inakuwaje wewe mlokole unasali na Mungu anashuka, mapepo yanatoka, lakini bado wewe una matatizo nyumbani kwako? Nakuambia, “Usiogope maana hali hiyo haitakuwa ya kwako milele maana Mungu yupo kazini atageuza kibao chako, atageuza matatizo yako, atageuza shida yako”. Maandiko yanasema, “Utazaa mtoto utamwita Yohana na baada ya kumwita Yohana furaha yako ya watu itakuwa juu yake yaani watu wengi watafurahia muujiza wako. 

Yamkini leo umekata tamaa huoni mlango wa kutokea, nakuambia, “usikate tama, baada ya haya mateso unayopitia watu watasherekea furaha yako, watu watashangilia hicho ulicho nacho, maana siyo wewe umesababisha ila Mungu anakupitisha hapo ili baaada ya hapo uwe na kitu cha kusema, “nimeuona mkono wa Bwana kwa sababu mahali nilipotoka na hapa nilipo ni Ebeneza kanitoa, ni Ebeneza kanisaidia”. Ishinde roho ya kukatisha tamaa.