RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.10.2016: ALICHOKINENA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE JUU YA IBADA YA MEZA YA BWANA SIKU YA JUMAPILI

Siku ya Jumapili 23.10.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare katika ibada ya Meza ya Bwana ambapo waumini wote wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” na wageni waliofika waliweza kula mwili wa Yesu Kristo na kunywa damu ya Yesu Kristo, alikuwa na haya ya kusema, “Sasa kaa na matarajio, leo tuna ibada  kubwa mbele yetu ni ibada ya meza ya Bwana, leo tunaenda kushiriki kwa pamoja meza ya Bwana, chakula cha mbinguni, chakula cha kiroho. 
Bishop  Dr. Gertrude Rwakatare akijiandaa kula mwili wa Yesu na kunywa damu ya Yesu 

Tunashiriki meza ya Bwana kwa sababu tunataka ufunguliwe. Kuna sababu mbalimbali za kushiriki
 meza ya Bwana  ambazo kama utazijua utashiriki meza ya Bwana kila siku. Kuna nguvu ndani ya damu ya Yesu, damu ya Yesu inafaida nyingi kwako, ni silaha kwako, itakuokoa na mambo mengi, ni ushidi, ni ulinzi. Katika siku za mwisho, Yesu Kristo alishiriki meza ya bwana na wanafunzi wake na akawapa agizo kwamba, “Fanyeni hivyo kwa ukumbusho wangu”.

Tunaposhiriki meza ya Bwana ni kwamba tunashiriki chakula cha mbinguni pamoja na Kristo, unapata uponyaji wako, kutumiwa kama chombo cha Kristo, lakini itatumika tu pale ambapo wewe utaichukua uitumie. wengi hawashiriki kabisa meza ya Bwana katika makanisa yao, lakini wale ambao wanafanya hivi kila mara Mungu anawabariki.

BISHOP DR. GERTRUDE ASHUHUDIA MCHAWI ALIVYOKUWA AKIMUWINDA
Mimi ni shuhuda hapa Mikocheni wakati tunaanza kanisa kulikuwa na wakati mgumu sana, kwa sababu kulikua hakuna makanisa kabisa, mahali hapa lakini wenzetu walikuwa na mahali pa kuabudia, lakini Mungu ni mwaminifu tulipoanza na darasa kuna mzee mmoja alikuwa ananitania kila asubuhi akisema, “Mwanamke wa Kipogoro umelalaje?” 
Namwambia, “Tumelala salama”, anasema, “Hakijatokea kitu chochote chenye moto?” Nikamwambia, “Moto hamna” nikagundua kumbe nikisema, “Damu ya Yesu inizunguke kumbe yeye katika uchawi anaona moto” Nikagundua kuwa kuna nguvu ndani ya Damu ya Yesu, ninapo lala nasema, “Damu ya Yesu nainyunyiza sehemu zote za nyumba yangu, watu wasinione watu wabaya”. Mwingine siku moja kaja akaniuliza, “Vipi mbona nimeona maji mengi hapo?” 
Nikasema “Maji gani?” Kumbe alikuwa anaona bahari yaani nyumba yangu anaiona mbele ya mto au upande mwingine wa mto. Mungu atakulinda isivyo kawaida, unaweza kuona kitu cha kawaida lakini damu ya Yesu ni silaha kubwa kupita silaha zozote katika ulimwengu wa Kiroho. Pia Wakorintho 5:7m inasema, “Itakulinda na mauti, itakulinda na mambo yote mabaya.

BISHOP DR. GERTRUDE ASHUHUDIA MZUNGU ALING’ATWA NA NYOKA NA KUPONA KIMUUJIZA
Mmisionary mmoja alikuwa amekuja Africa kumtumikia Mungu, akaingia katika kijiji fulani akihubiri Neno la Mungu, nyoka akamng’ata alivyokuwa ameng’atwa mahali pale palikuwa hakuna daktari, wala hakuna dawa lakini akaushika ule mguu wake, akasema, ”Damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani kwaajili yangu katika jina la Yesu nimepona na kila sumu haitatua kwangu”. 
Alivyosema hivyo kukotokea maji, kama bakuli hivi zima ya maji kama nusu ndoo ikamwagikia kwenye ule mguu uliong’atwa na nyoka badae akaona kitu cheusi kimetoka kama damu, watu wakasema, “Yule nyoka haachi mtu, yule mzungu lazima afe”, lakini wakaona mtu kapona na maji yametoka. Mungu alimponya, unajua maji ni damu ya Yesu pia maji ni uhai kwahiyo yule mzungu alimshinda shetani kwa damu ya mwanakondoo pamoja na ushuhuda. 
Bwana hakika anaweza kukulinda, anaweza kukupa ushindi wa mambo mbalimbali, ukipata ushindi wa kushinda dhambi utakuwa katika mikono salama ya Mungu. Wengi walikuwa walevi, watu wengi walikuwa na tabia mbaya lakini alipokwisha kuokoka walipata mabadiliko makubwa kwa sababu ya damu ya Yesu inakata kiu ya dhambi zile za zamani na ndio maana watu wa dunia wanashangaa,

JE, INAWEWZEKA KUISHI BILA MKE AU MUME WAKATI NDANI YAKO KUNA DAMU YA YESU? BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ASHUHUDIA MWANAE KUACHA ULEVI, ONDOLE KUACHA ULEVI BAADA YA KUWAOMBEA

Watu wengi sana siku hizi imani yao imeshuka, utasikia wakisema “Haiwezekani mwanaume mzuri hivi anaweza kuishi bila mshikaji?” Kweli unaweza kuishi bila mshikaji? Mwanaume huyu anaweza kuishi kwa sababu ndani yake kuna damu ya Yesu inayomtetea, inayompa nguvu ya kushinda majaribu ya dhambi. Watu wa dunia hawaamini kwa sababu wao wanashindwa lakini tulio katika Kristo damu ya Yesu inaweza kutushindia.
 Unakuwa na matamanio mapya ya msingi katika maisha yako, unaanza kutamani Ibada, harusi, mkesha, Neno la Mungu, watumishi wa Mungu, kuhubiri, kujiheshimu n.k kwasababu damu ya Yesu imekupa nguvu ya kuendelea mbele, endelea kushiriki meza ya Bwana, na tunaposema meza ya Bwana tamani kutokosa ibada kwa sababu damu ya Yesu ni ukombozi inatukomboa na mambo mbalimbali. 
Nakumbuka wakati nalia kwa jili ya mtoto wangu Hamfred asitumie pombe, nilikuwa nasema, “Mungu naomba nisaidia huyu ndiye mtoto wangu wa kwanza namtegemea, Mungu angalia amekuwa mlevi, damu ya Yesu mkomboe mwanangu”. Namshukuru Mungu damu ya Yesu ikamkomboa, na siku moja nikasikia anasema, “Mimi sinywi tena pombe”, nikamuuliza, “Mbona sisikii ile harufu yako ya pombe tena?” Akasema, “Mimi nilishaachana nayo”.
 Jamani Mungu anaweza kubadilisha, kukukomboa wewe na watoto wako walevi. Pia nashukuru Mungu pia kwajili ya Utua mtoto wangu “Ondole” kwani tumeomba sana kwa ajili yake na mama Elizabeth Lucas, sasa Mungu amemkomboa na ulevi na sasa hivi ni mtumishi. SOMO LILIENDELEA