RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ANTÓNIO GUTERRES NDIYE KATIBU MKUU MPYA WA UMOJA WA MATAIFA

António Manuel de Oliveira Guterres.

António Manuel de Oliveira Guterres, alizaliwa Aprili 30, 1949 jijini Lisbon, Ureno. Ana familia yenye watoto wawili Pedro na Mariana. Alianza siasa mwaka 1974 alipojiunga na Chama Cha Socialist Party.

Mwaka 1992 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama chake. Mwaka 1995 chama chake kilishinda uchaguzi mkuu nchini Ureno, ushindi wa chama chake ulimpa nafasi ya kuwa Waziri Mkuu kuanzia mwaka 1995-2002. Aliweka rekodi nzuri kwenye awamu yake ya kwanza hali iliyopelekea kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1999. …Alipotembelea kambi ya wakimbizi nchini Kenya.

Awamu ya pili haikuwa nzuri kwake baada ya kuibuka kwa mgogoro mkubwa ndani ya chama chake, aliamua kujiuzulu nafasi yake Desemba 1, 2001 na kumlazimisha Rais Jorge Sampaio kuvunja baraza la mawaziri na bunge na kuitisha uchaguzi mwingine. Alijihudhuru mambo ya siasa za Ureno mwaka 2005.

…Akisitiza jambo.

Mei 2005 alichaguliwa kuwa Kamishna wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya wakimbizi. Aliweza kuongoza na kusimamia wafanyakazi zaidi ya 10,000 waliotawanyika nchi zaidi ya 126 duniani kote wakiwasaidia wakimbizi zaidi ya milioni 60.

Katibu Mkuu wa UN anayemaliza muda wake, Ban ki-moon.

Huyu ndiye atakuwa mrithi wa Katibu Mkuu wa UN anayemaliza muda wake, Ban ki-moon.