RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ARUSHA: HUKUMU YA KESI YA OLE NANGOLE YAAHIRISHWA


Mahakama ya Rufaa Tanzania, Arusha leo Oktoba 24, 2016 ilitarajiwa kutoa uamuzi wa rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Longido, Bw. Onesmo Ole Nangole lakini hukumu hiyo imeahirishwa hadi pale mkurugenzi wa uchaguzi pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali watakapowekwa kwenye rufaa hiyo.

Hakimu aliyekuwa akisoma rufaa hiyo John Kahyoza ambaye alikuwa akisoma hukumu hiyo ametoa siku 21 kwa upande wa wakata rufaa kurekebisha taarifa yake ya rufaa ndani ya siku hizo.

Awali Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitengua ubunge wa Bw. Onesmo Ole Nangole kutokana na kujaza matokeo ya ubunge kwenye fomu ya udiwani

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido, Dkt Steven Kiruswa alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido Onesmo Nangole.