MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BENNY WILLIAM NA NDOTO ZA KUUBADILISHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA KWA KUINUA VIPAJI VIPYA.
Mwimbaji nyota wa Muziki wa Injili Tanzania Benny William amezidi kung’ara kutokana na kazi zake anazozifanya za kuinua waimbaji wanaotaka kuimba na hawana uwezo wa kutunga ama pesa za kurekodia hawana.

 Alisema kwamba licha ya yeye kuwa mwimbaji lakini anafahamu kuwa nyuma yake kuna kundi kubwa la watu wanaotamani kuimba lakini hawana uwezo wa kifedha na wengine hata uwezo wa kuzitunga nyimbo pia hawana hivyo ameamua kulibeba jukumu hilo awasaidie waimbaji wanaotamani kuimba kwa kufungua studio kubwa na ya kisasa kwa ajili yao.

”Moyo wangu huwa unaumia sana pale ninapoona watu wanatamani kuimba halafu hawana uwezo hicho kitu huwa kinaniumiza sana kiasi kwamba hata mimi hivi nilivyo ni kwa Neema tu ya Mungu maana kuna watu wana uwezo wa kuimba sana tu ila hawajapata Platform ya kutosha, pia nitaanza darasa la vocal training mwezi ujao nita wanoa watu na watarekodi bure bila malipo baada ya studio yangu kukamilika maana ipo hatua za mwishoni pia darasa litakuwa la miezi miwili tu na litaanza jingine na nitawajulisha lini tutaanza rasmi”Alisema Benny William.

Mwimbaji huyo mahiri wa miondoko ya RnB anayetamba na Nyimbo zake kama Surprise na Wonders yupo njiani kufanya Collabo kubwa na Mkali mwenzie wa miondoko hiyo hivi karibuni.

Pia Benny anawatungia nyimbo waimbaji mbalimbali hapa nchini wa Gospel, mbali na uimbaji pia ni Producer na ni mwalimu wa sauti.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Benny William kupitia
Simu/WhatsApp: +255 719 813 124 au +255 754 065 514
Facebook: Ben William
Instagram: @benwilliam
YouTube: Beatrice Kitauli
Email: benwillilam307@gmail.com