MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE NA KANISA ZIMA WAFANYA MAOMBI MAALUM KWA MTUMISHI WA MUNGU MWENYE TATIZO LA KIBOFU

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji unaoendelea kwa huyu mtumishi wa Mungu ambaye alifika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwaajili ya maombezi kutokana na tatizo la kibofu. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kanisa zima waliweza kumuombea. Maombi haya yalifanyika siku ya Jumapili 25.09.2016 katika kipindi cha Maombezi na Uponyaji.

Tunahitaji sana maombi yako kwaajili ya huyu ndugu yetu ili awe mzima na aendelee na majukumu yake kama awali. Maombi yako ni ya muhimu sana katika afya ya huyu mtumishi wa Mungu.

Tunakukaribisha pia katika ibada zetu za kila Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kutoka katika kituo cha Mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utayaona magari ya Mlima wa Moto au utasikia watu wakisema, "Kwa mama". Ingi humo na utafikishwa salama.