MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WAUMINI WAPYA WALIVYO BATIZWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI 25.09.2016

Siku ya Jumapili 25.09.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliwaombea na kuwaongoza sala ya toba waumini wapya walioamua kuokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao 

Baada ya maombezi walipelekwa baharini kubatizwa kwa maji mengi na baada ya hapo Siku ya Jumanne walianza masomo ya kukulia wokovu.

Kipindi wanabatizwa kuna baadhi yao walitokwa na mapepo, majini na nguvu za giza wakati watumishi wa Mungu wakiwaombea. Pia waliweza kujazwa Roho Mtakatifu. 

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa jinsi anavyofanya maajabu na matendo makuu katika huduma hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Pia tuna kila sababu ya kuwashukuru wachungaji, wainjilisti, wahudumu na waumini wa kanisa hili kwa juhudi zao wanazo fanya kuokoa Roho za watu kupitia mafundisho yao, ushauri wao na kuwatia moyo ndugu zetu ambao wameamua kuokoka.

Tunakukaribisha Jumapili hii katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi na usafiri ni bure kutoka kituo cha Makumbusho na Mwenge.

Tembelea www.mountainoffiretanzania.blogspot.com