RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BURUNDI IMEAMUA KUSITISHA USHIRIKIANO WAKE NA UN KUHUSU HAKI ZA BINADAMU


Jumanne ya October 11, 2016 Nchi ya Burundi imezimiliki headlines nzito baada ya serikali ya nchi hiyo kuchukua uamuzi wa kusitisha ushirikiano wake na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, kwa kile inachodai kuwa ofisi hiyo imekuwa ikiihujumu serikali yake wakati wa kuandaa ripoti ya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa (EINUB).


>>>Kufuatia njama ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu nchini Burundi, katika maandalizi ya ripoti ya uongo na yenye utata ya Wataalam wanaodaiwa kufanya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi (EINUB), Serikali ya Burundi imeamua kusitisha ushirikiano wowote na kushirikiana katika miundo yake yote, pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binanadamu hadi itakapotangazwa tena:- Imesema taarifa hiyo


Maneno haya yameonekana kwenye tangazo lililosainiwa Jumanne hii Oktoba 11, 2016 na Philippe Nzobonariba, ambaye ni katibu na Msemaji wa serikali. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo uliripotiwa muda ambao maofisa wake wakiwa kwenye kikao cha kazi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe, Jumatatu ya Oktoba 10, 2016.

>>>Kwa maana hii, Burundi inaomba kwa kusubiri, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuteua timu itakayoendesha mazungumzo kuhusu makubaliano ya makao makuu, ambayo yataweka wazi majukumu yake, muda na idadi ya wafanyakazi wake nchini Burundi:- Imeongeza taarifa hiyo.


Uamuzi huu unakuja baada ya maandamano mjini Bujumbura mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya makao makuu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambapo waandamanaji waliomba ofisi hiyo kufungwa haraka iwezekanavyo.

Ripoti ya EINUB ilikuwa chanzo cha azimio la HRC33 lililochukuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo linaomba kuundwa kwa Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi wa ukiukaji wa haki zabinadammu nchini Burundi. Azimio ambalo lilikataliwa na serikali ya Burundi, ambayo inautuhumu Umoja wa Ulaya kuwa imeandaa na kupanga njama dhidi yake.