RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DK. KIGWANGALLA KUONGOZA MATEMBEZI SARATANI YA MATITI OCEAN ROAD

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage akizungumza na wanahaba (hawapo pichani).

Mkurugenzi Mtendaji wa Mkoa wa Hospitali ya Agha Khan, Sulaiman Shahabuddin (kulia) naye akifafanua jambo katika mkutano huo.

Ofisa Mauzo wa Hoteli ya Kunduchi Beach, Winnie Kimotho (katikati) naye akipata fursa ya kuzungumza jambo.Mkutano na wanahabari ukiendelea.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika matembezi ya hisani ya kuongeza uelewa wa chanzo na athari ya saratani ya matiti na kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba.

Matembezi hayo yameandaliwa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hoteli ya Kunduchi Beach na Hospitali ya Agha Khan za jijini yanayotarajia kufanyia Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage amesema leo kuwa matembezi hayo yataanzia katika taasisi hiyo saa 12.30 asubuhi na kuhitimishwa saa 4,30 yakielenga kuongeza uelewa wa chanzo na athari ya saratani ya matiti na kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya chemotherapy, hivyo kuchangia juhudi za serikali katika tiba ya saratani hiyo hapa nchini.

Alifafanua kuwa ugonjwa wa saratani ya matiti umekuwa ukiongezeka siku hadi siku duniani kote, ongezeko hilo likiwa kubwa zaidi katika nchi zinazoendelea kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani mwaka 2012 zilizoonyesha kwamba kila mwaka wagonjwa wapya milioni 14.1 hugundulika, kati yao milioni 8.2 wakifariki dunia na kuchukua

idadi ya asilimia 13 ulimwenguni kote.
“Hapa nchi idadi ya wagonjwa wapya kila mwaka ni takribani 44,000 lakini wengi wao kwa sababu mbalimbali hawafii hospitalini na ni asilimia 12.5 ya wagonjwa ndio wanaofika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu na matibabu.

“Takwimu zinaonyesha kuwa saratani ya matiti ndiyo inayoongoza duniani kote kwa wanawake kuwa na wagonjwa wapya milioni 1.7 wanaogundulika kila mwaka ukilinganisha na wagonjwa wapya 500,000 kila mwaka wanogundulika kuwa na saratani ya shigo ya kizazi,” alisema Mwaiselage.

Vilevile alibaisha kuwa kwa hapa nchini wagonjwa wa saratani ya shigo ya kizazi ni wengi zaidi kuliko wagonjwa wa saratani ya matiti kwa sababu mbinu za uchunguzi wa saratani ya kizazi ambazo zimekuwa zikitumika kwa miaka 50 iliyopita zimechangia sana kupunguza tatizo hilo katika nchi zinazoendelea lakini kwa hapa nchini mbinu hizo zimeanza

kutekelezwa hivi karibuni.
“Ili kuondokana na tatizo hili serikali imeanza kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kuzuia na kudhibiti saratani kwa kuongeza juhudi za upimaji wa dalili za saratani pia kutoa chanjo dhidi ya kirusi cha HPV kwa wasichana, ” aliongeza.
Aidha wadau mbalimbali wametakiwa kujumuika siku hiyo ili kuwezesha zoezi hilo la hisani kwenda vizuri, huku akitaja namba kwa mtu atakayehitaji kuchangia anaweza kutuma katika namba 0719 803 344 au M.PESA 175555