MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

EMMANUEL KUTOKA MUSOMA APOKEA UPONYAJI WA MIGUU NA KISUKARI: 25.09.2016

Ninamshukuru Mungu sana. Roho yangu inaogopa na kutetemeka kwa uwezo wa Mungu. Mungu aliye niumba sasa nimegundua kuwa ndie aananipenda. Nimesumbuliwa na mguu wangu takribani miaka 20 na ndio ulionitoa Serengeti, Mara nikaja dar es Salaam kwa matibabu pamoja kupimwa na macho, figo na moyo. Kufika kwangu Mlima wa Moto Mikocheni “B” ni muujiza wa Mungu, nililetwa na Rose. Rose alinikuta njiani nikihangaika kwenye basi, kwababu basi nililopanda walinipitiliza kituo. Rose akaniona nikiomba “lift” ya pikipiki ili nifike kituoni, Rose ananiambia, “Wee..!! mzee unaonekani ni mgeni unaweza ukagongwa na magari?”. Nimekufuata twende kanisani Mlima wa Moto Mikocheni. Nikamuangalia Rose kama nafahamu, lakini kumuangalia simfahamu, nikasema, “Yawezekana kuna kitu ngoja nimsikilize”, akaniuliza, “unaenda wapi aun unaenda kanisani?” Nikamuelekeza ninakokwenda, akasema, “twende ntakulipia nauli” nikasikia Roho wa Mungu akiniambia, “si umsikilize huyu mama basi” nikaondoka nae kwenda anaposali, akaninunulia chakula. Badae akaniuliza, “unaenda wapi?” nikamjibu, akanipa namba ya simu. Rose akasema “sasa tunaenda kusali kwa mama Rwakatare”, nikamkubalia, nilipofika nikaombewa. Miguu yangu hii imeathiriwa na kisukari nikaombewa. Jumapili ya 25.09.2016, lakini mpaka leo nasikia uponyaji. Uweza wa Mungu ni waajabu mtafute Mungu kwa kumaanisha Mungu anatupenda kuliko tunavyojua, tuendelee kumwombea Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kazi anazo zifanya Mungu awabariki sana.