RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EUNICE MTAVANGU: NAFSI YANGU




Shalom! Kutoka Iringa Tanzania tovuti ya gospomedia.com leo inakukaribisha kuitazama video mpya kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki wa Injili, huyu si mwingine bali ni EUNICE MTAVANGU ambaye leo ameachia video yake mpya ya wimbo unaokwenda kwa jina la NAFSI YANGU ikiwa imeongozwa na director Shama Kilasi na audio ya wimbo huu ikiwa imetengenezwa ndani ya studio ya Shekinah Records, chini ya mikono ya producer Amani.
Akiongea na GospoMedia.com mwimbaji Eunice Mtavangu amesema kuwa wimbo huu ni wa kuabudu na ameachia video hii rasmi ili kuwaleta watu karibu na uwepo wa Mungu ili waweze kutakaswa na kubarikiwa nafsi zao kwa kutudumisha uhusiano wao na Mungu kupitia sala(Maombi), toba na sadaka ikiwa ni msingi mkuu kwa wote waaminio kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo hivyo ndivyo alivyofunguka mwimbaji Eunice Mtavangu kuhusu video ya wimbo huu.
gospomedia.com tumekuwekea video ya wimbo huu wa NAFSI YANGU uweze kuitazama na kuupakua(kuudownload), kuusikiliza na kuwashirikisha wengine kwa kadri uwezavyo ili kumpa sapoti mwimbaji Eunice Mtavangu na hakika utainuliwa na kubarikiwa sana… Karibu!!
Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Eunice Mtavangu kupitia
Simu/WhatsApp: +255718985615
Facebook: Eunice Mtavangu
Instagram: @eunicemtavangu
Youtube: eunice mtavangu