MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

JENGO JIPYA LA JULIUS NYERERE LAZINDULIWA NA KANSELA ANGELA MERKEL, ETHIOPIA


ADDIS ABABA, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani leo amezindua jengo jipya la amani la Umoja wa Nchi za Kiafrika (AU) lililopewa jina la Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kansela Merkel na Nkosazana Dlamini-Zuma.

Jengo hilo lililojengwa kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani na kujengwa na Kampuni ya Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) lipo kwenye makao makuu ya AU yaliyopo jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Akizindua jengo hilo mbele ya Rais wa AU, mwanamana Nkosazana Dlamini-Zuma, Kansela Merkel amesema:

“Ni lazima sasa AU iingilie na kuweka sawa hali ya usalama nchini Libya. Nipo tayari kutoa mchango wangu kwenu ili kuhakikisha hali ya kiusalama inaimarika Libya na nchi nyingine zenye migogoro.”

KWA NINI LIMEPEWA JINA LA JULIUS NYERERE?Nyerere (katikati), Kaunda (kulia) na Samora Michelle (kushoto).

Julius Nyerere ni kielelezo cha uhuru wa Afrika, alichangia kupatikana kwa uhuru wa nchi nyingi Kusini mwa Jangwa la Sahara zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Namibia, Afrika Kusini na Angola.

Alisimamia na kufanikisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, muungano ambao umedumu mpaka leo.

…Akisimamia zoezi la kuchanganya udongo kama ishara ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, 1964.

Alisimamia mazungumzo ya amani ya nchi zenye migogoro barani Afrika.

Wazo la kulipa jina la Mwalimu Julius Nyerere jengo hilo, lilianzia kwenye kikao cha kamati ya amani ya AU iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Peter Katjavivi ambaye kwa sasa ndiye Spika wa Bunge la Namibia.

Walipendekeza wazo la kuyapa majina maeneo maarufu ya ukombozi yaliyosimamiwa na Nyerere nje ya Tanzania na kwa kuanza waliyapa majengo ya ukombozi jijini Harare, Zimbabwe jina la Mwalimu Julius Nyerere.

Kwenye sherehe hiyo iliyofanyika jijini Harare, mgeni rasmi alikuwa Benjamin William Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mkapa alisema:

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

“Tunafahamu umuhimu wa historia kwa jamii yetu, siyo kwa wapinzani wetu tu na wafuasi wao bali kwa wote waliosimamia ukombozi wa bara letu.

“Mwishoni mwa miaka ya sabini, tulipokuwa na uhakika wa nchi zetu kupata uhuru, ikiwa ni pamoja na kutumia uhuru huo kujikwamua kiuchumi na kuwa kama wao, juhudi kubwa zilifanywa na viongozi wetu ambao pamoja na vitisho walidhamiria kushinda.

“Kuyapa majengo haya jina la Nyerere ni dhahiri mchango wake wa kupambana na ukoloni uko wazi na unatambulika hata nje ya Tanzania ikiwemo hapa Harare.”

Baada ya hotuba ya Mkapa, Mkurugenzi wa Amani wa Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Phyllis Johnson alisema wanajivunia kuwa sehemu ya mawazo ya Mwalimu Nyerere na kupendekeza jengo jipya la amani liitwe kwa jina la Nyerere.

Wazo hilo lilipelekwa kwenye mkutano mkuu wa AU mwaka 2015 ambapo wajumbe wote waliunga mkono makao hayo kuitwa jina la Mwalimu Julius Nyerere. Hatimaye leo limezinduliwa rasmi na kuitwa jina la Mwalimu Julius Nyerere.