RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JESCA AMSHUKURU MUNGU KUPONA VIDONDA VYA KOO: 25.09.2016

Nikuja Mlima wa Moto Mikocheni “B” nikisumbuliwa na koo, nilikuwa siwezi kula chakula, chakula changu kilikuwa ni maji labda na ugari mwepesi, vyakula vingine nikila nilikuwa kama vimemwagiwa pilipili kwenye kidonda. Nilikuwa naacha kula nalala njaa. Siku moja nilikuwa na marafiki zangu watatu nikawambia kuwa nimeenda hospitali nimepewa dawa na nimechoma sindano lakini sijapona na sijapata nafuu yoyote. Tulikuwa tunaongea tu kwenye maongezi ya kawaida. Mara tukawa tunasema tuje kanisa la Mlima wa Moto. Nikawaambia marafiki zangu kuwa kesho nishapanga kwenda hospitali, sasa kama ninyi mnaenda kanisani basi sitaenda hospitalini ila tuongozane kanisani kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Marafiki zangu wakanambia, “ukiwa na imani unaweza kuombewa na ukapona.” Jumapili 18.09.2016 nikashiriki ibada na walivyoanza kusema, wale wenye vidonda kwenye titi waje mbele maana uponyaji wao umekaribiwa” kikamwambia mama aliyekuwa jirani yangu katika ibada, “mimi vidonda vyangu vipo kwenye koo siyo kwenye titi” akaniambia, “nenda ukaombewe madhabahuni” ndio nikaja mbele kuombewa. Namshukuru Mungu sana sasa hivi ni mzima nimepona nakula kila kitu namshukuru Mungu sana. Nilikuwa nashindwa kufanya kazi zangu maana natetemeka, njaa inauma siwezi kula chochote 

Huu ni ushuhuda wa Jumapili 25.09.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B