MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

16.10.2016: WATU WAZIDI KUBATIZWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 16.10.2016 watu wengi walijitokeza madhabahuni kuyakabidhi maisha yao kwa Yesu. Mch. Francis Machichi na Mch. Elizabeth Lucas waliwaongoza sala ya toba na kuwaombea. Baada ya kuombewa walibatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumanne walianza masomo ya kukulia wokovu. Sasa ni zamu yako wewe kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare pamoja na jopo la wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” wanakubaribisha katika ibada ya Jumapili hii kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 8 mchana, na siku za katikati ya wiki ibada zinaanza saa 9 mchana hadi usiku isipokuwa Jumamosi. Mungu anampango na wewe katika maisha yako, amua sasa kuishi maisha yanayompendeza Mungu alafu utaona mkono wake ukikugusa na kubadiliza Historiya ya maisha yako. Jinsi ya kufika kanisani fika kituo cha Makumbusho au Mwenge utaona mabasi ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” au utasikia watu wakisema “kwa mama”.  Mungu akubariki sana.