RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KAMANDA SIRRO APOKEA HUNDI YA MILIONI 50


Mkurugenzi wa shirika hilo kupitia Kitengo cha Idara ya Uhusiano na Masoko NSSF, Godius Kabyara (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh, 50,000,000 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, CP Simon Sirro.

Kamanda Sirro akipokea hundi halisi ya Sh. 50,000,000.

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, CP Simon Sirro leo amepokea msaada wa hundi ya Shilingi 50,000,000 kutoka mfuko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kusaidia ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kiluvya-Gogoni Dar.

Msaada huo umetolewa na mkurugenzi wa shirika hilo kupitia Kitengo cha Idara ya Uhusiano na Masoko NSSF, Godius Kabyara katika Ofisi za Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kabyara alisema kuwa msaada huo umetolewa kwa mujibu wa sera za shirika katika kuisaidia jamii kwenye nyanja za elimu, afya, mazingira, michezo na maeneo mengine yaliyopo kwenye sera yao.

Alifafanua kuwa NSSF imeona ni vyema ishiriki katika suala zima la kuhifadhi na kulinda jamii na mali zao kwani jamii hiyo ndio ambao shirika linaitegemea kulichangia na kisha kutoa mafao kwake kwa mujibu wa sheria za hifadhi ya jamii.

Aliongeza kuwa mbali na kulichagia kwenye ujenzi huo pia NSSF miaka michache iliyopita liliwezesha ujenzi wa nyumba za polisi kwenye Mkoa wa Dar na Visiwani Pemba, Zanzibar.

Naye Kamanda Sirro alilipongeza shirika hilo kwa kutambua na kuthamini michango inayotolewa na jeshi la polisi katika jamii, akasema kuwa anawashukuru kwani anaamini fedha hizo ni nyingi na zitawezesha kujengwa kwa kituo hicho ambacho kitakuwa cha wilaya, akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo.