RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA UJENZI WODI ZA WAZAZI


Makamu wa Rais, Samia Suluhu akizindua jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dar.Baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kushuhudia hafla hiyo. Makamu wa Rais (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliofika katika hafla hiyo.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo amezindua mradi wa ujenzi wa majengo matatu ya wodi za wazazi wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 kwa Halmashauri tatu za jiji la Dar es Salaam.

Mradi huo wa ujenzi ulizinduliwa katika Hospitali za Rufaa za Mwananyamala (Kinondoni) , Amana (Ilala) na ile ya Temeke .

Akizungumza katika hafla hiyo, Samia Suluhu alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi zake katika kutafuta wadau mbalimbali na kufanikisha kujitolea kujenga majengo hayo ambayo yatakuwa muhimu kwa wazazi mkoani Dar. Pia alimshukuru Mkurugenzi wa Amsons Group, Abdallah Naheer kwa kukubali kujenga majengo hayo yatakayopunguza vifo vya akina mama na watoto.

Kwa habari kamili tembelea Global TV Online kuona hotuba kamili ya hafla hiyo.

Na Denis Mtima/Gpl