MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MAREHEMU WINNIE JACKSON BENTY KUZIKWA NJIRO, ARUSHA TAREHE 11.10.2016.


Heshima za mwisho kuuaga mwili wa marehemu Winnie Jackson Benty ama Mrs Benty ambaye ni mke wa muimbaji wa nyimbo za injili na kiongozi wa sifa Kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha, Jackson Benty zitafanyika Jumanne ya tarehe 11.10.2016, maeneo ya Njiro mkoani Arusha. Msiba huu umewekwa nyumbani kwa marehemu, Kwa Mrombo karibu na bomba la maji ya jeshi Arusha.

Chanzo cha taarifa kimeeleza kwamba marehemu Winnie Jackson Benty alikutwa na umauti sehemu inayoitwa Burka, Jijini Arusha kutokana na ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Mtei Express na pikipiki aliyokuwa amepanda.

Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mount Meru, ambapo ibada ya mazishi itaanza saa tano asubuhi hadi saa saba mchana kisha kufuatiwa na msafara wa kwenda makaburini, Njiro Arusha.

Kutoka kushoto ni muimbaji Jackson Benty akiwa anafurahi na familia yake katikati ni mtoto wao na kulia ni mke wake ambaye sasa ni marehemu Winnie Jackson Benty.

Marehemu Winnie Jackson Benty ameacha mjane na watoto wawili, mkubwa akiwa na umri wa miaka mitano.
Marehemu Winnie Jackson Benty akiwa na mtoto wake kipindi cha uhai wake.

Hakika hili ni pigo kubwa kwa Tasnia ya muziki wa Injili Tanzania kwa kaka yetu Jackson Benty kuondokewa na Mke wake Winnie Jackson Benty, kwa wakazi wote wa Arusha unaweza kufika msibani nyumbani kwa Jackson Benty kwa mrombo karibu na bomba la maji la jeshi kumtia Moyo, lakini pia kama upo mbali na umeguswa na msiba huu, Tunaweza Kutuma rambirambi zetu kwa MPESA +255754295801 ili kumtia moyo ndugu yetu Jackson Benty aliyefikwa na msiba huu.

Uongozi na timu nzima ya gospomedia.com tunatoa pole ya dhati kwa muimbaji wetu Jackson Benty kwa msiba huu tunaamini Mungu atakwenda kumtia nguvu kubwa ya Imani katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu, BWANA ametoa na BWANA ametwaa jina la BWANA lihimidiwe.