RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

16.10.2016: ELIZABETH LUCAS AFUNDISHA JUU ROHO MTAKATIFU KATIKA KIPINDI CHA SUNDAY SCHOOL JUMAPILI

FAIDA ZA KUFUNGA
Siku ya Jumapili 16.10.2016 Mch. Elizabeth aliweza kufundisha juu ya Roho Mtakatifu na sehemu ya somo hili alikuwa na haya ya kusema; Watu wanaiogopa kufunga kwa kuogopa njaa, lakini mwisho wa njaa yako ni kupata hasara, sasa ukubali kuutesa mwili wako kwa kufunga na hatimaye ufunguliwe katika mambo magumu. 
Biblia inasema, “Hatulegei japokuwa utu wetu wa nje unachakaa”. Kiukweli ukifunga unaweza ukaonekana unanyong’onyea, katika hali fulani lakini jua ya kwamba mwili na damu havitaurithi ufalme wa Mungu. Biblia inasema, “Ijapokuwa mwili wa nje unachaka, mwili wa ndani unakuwa na nguvu”, kwahilo ile nguvu unayoipanda ndiyo inaweza kukuondolea kile ambacho Roho Mtakatifu amekufunulia. 
Roho Mtakatifu atakuonyesha mambo ya sirini, mambo ambayo yalikuwa yakumalize kabla, kama vile mchawi alipanga akuangamize atashangaa anasema, “Huyu ni mchawi, alijuwaje kama mimi nilikuwa nimemkusudia nimloge?” Amejua kwa sababu yupo mtu ndani yetu. 
Yesu ambaye anajua, anapambana vita ndio maana kasema, “Nitamuomba Mungu awaletee msaadizi mwingine”, yeye akiondoka Yesu atamleta Roho Mtakatifu huyu ndiye anayetusaidia katika vita. Tukishirikiana na Roho Mtakatifu katika kuomba atatusaidia na kutupa maombi yenye nguvu, halafu yatamgusa Mungu sababu tutaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. 
Kama kuna kitu kibaya, hali ngumu ya kiuchumi Bwana anasema, “Ataiamuru baraka ikujilie” Baraka itakuja kwako ikuwezeshe kutoka kwenye hali ngumu ya kimaisha. Hata kama unashida jua kuwa wakati unakuja na mimi nitakula nyama choma, nitakuwa na mume wangu mwenyewe.

Wakati unakuja nami nitashika pesa zangu mkononi sitakuwa mtu wa kukopakopa maana maandiko yanasema hivi, “Hatutakopa bali tutakopesha, hatutakuwa mikia bali tutakuwa vichwa” hilo ni neno la Mungu linasema, “Siku zote Bwana aliwajua aliowachagua, watasimama katika dunia na kuudhihirisha uwezo wa Mungu, watakuwa vichwa, watasimama kumtetea Bwana, watashuhudia kuwa niliokoka nikiwa na ninakandambili tu lakini leo naendesha gari, nakakula dagaa siyo kwa kupenda bali sina pesa ya kula sembe nzuri”, lakini huyu Mungu tunaye muhubiri ndiye awezaye kutengeneza milango ya Baraka, ndiye anaye weza kuondoa aibu ya mtu wake, ukitaka aibu ni wewe mwenyewe lakini Yesu amesema, “Atasimama atakua, ni mtetezi wako na hutapungukiwa”. Bwana wa mabwana asema hivyo, cha msingi vuta subira, Mungu ni mwaminifu.


HASARA ZA KUTOSHIRIKIANA NA ROHO MTAKATIFU

1. Maombi yako yanakuwa makavu hayana nguvu ya Mungu, hivi mnajua kitu kikavu? Nguo yangu ikiwa kavu nimeifua imekaa juani muda mrefu lazima ninapotaka kunyosha ninyunyuzie maji ili iwe laini. Maombi yako yatakuwa makavu yaani hayana nguvu ya Mungu yaani yapo yapo tu kama hauna Roho wa Mungu ndani yako. 
Utakuwa unaomba kwa kutafunatafuna tu maneno kwa maana unaomba kidini kidin,i maana yake huna roho ndani yako. Maombi yanayoongozwa na Roho Mtakatifu yanatanguliwa na kuubutu, unakaa mbele za Bwana unaanza kuabutu, nakwabudu, unaanza kusema, “Bwana ndiwe Bwana huku ukibubujika” utaanza kusikia uwepo wa Mungu unashuka. 
Lakini mtu ambaye hana roho wa Mungu ndani yake, anaingia kikavukavu, utasikia anasema, “Mungu unajua mimi sithaminiwi na maneno ya manung’uniko”, anaanza kumulaum Mungu lakini leo tafuta roho wa Mungu ili uweze kuwa na maombi yanayomgusa Mungu katika kiti chake cha enzi mpaka Mungu anaanza kuseme, “Hakika kuna mwanangu kanisa la Mlima wa Moto mikocheni “B” ananijua mimi Mungu wake”.

2. Hutaweza kuomba kwa muda mrefu kwa sababu huna kiongozi wa maombi, huna nguvu ya Mungu ndani yako. Yupo anayekuwezesha kuomba kwa muda mrefu, si kwa nguvu zetu, wala kwa uwezo wetu, bali kwa roho wa Bwana. 
Tutaomba kwa muda mrefu lakini pia huwezi kupokea ufunuo wa mambo ya siri ukiwa hushirikiani na Roho Mtakatifu katika kuomba. Nakupa pole kama umempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako alafu unasema maisha kwenye wokovu yamekuwa magumu ni kwako wewe lakini sisi tunashuhudia mambo mema anayoyatenda Yesu ndani ya maisha yetu.